IQNA

Mauritania haina mpango wa kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni

15:22 - September 02, 2021
Habari ID: 3474249
TEHRAN (IQNA) - Serikali ya Mauritania imekanusha madai ya kuwasiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa ajili ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia.

Waziri wa Utamaduni na Msemaji wa Serikali ya Mauritani Mokhtar Ould Dahi  ametoa kauli hiyo kujibu madai ya vyombo vya habari vya Utawala wa Kizayuni wa Israel ambavyo vimeandka kuwa, utawala huo umewasiliana na nchi kadhaa za Kiarabu na Kiislamu na kwamba Mauritania ni kati ya nchi hizo.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimechapisha ripoti siku ya Jumatano na kudai kuwa, mawasiliano na nchi hizo za Kiarabu na Kiislamu yalihusu uanzishwaji uhusiano rasmi wa kidiplomasia baina ya utawala huo na nchi hizo.

Ikumbukwe kuwa, mwaka 1999, Mauritania ilikuwa imeanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni lakini uhusiano huo ulivunjwa mwaka 2009 kufuatia amri ya rais wa wakati huo Mohammad Ould Abdulaziz baada ya utawala wa Kizayuni kuanzisha vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza. 

Mauritania ni nchi ya eneo la Maghreb huko kaskazini- magharibi mwa Afrika Kaskazini na inakadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 4.7 ambao karibu wote ni Waislamu.

Katika miezi ya hivi karibuni Umoja wa Falme za Kiarabu, Sudan na Morocco zilianzisha uhusiano rasmi na utawala wa Kizayuni wa Israel hatua ambayo inaendelea kulaaniwa vikali kote katika ulimwengu wa Kiislamu. Nchi zingine za Kiarbau zenye uhusiano rasmi wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel ni Misri na Jordan

3994657

captcha