IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mauritania kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Qur'ani Afrika Magharibi

15:51 - June 10, 2022
Habari ID: 3475358
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya kila mwaka ya Qur'ani Tukufu na Sunnah ya Mtume Muhammad SAW ya Afrika Magharibi yatafanyika nchini Mauritania.

Kwa mujibu wa taarifa mashindano hayo yamefadhiliwa na yanasimamiwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia kwa ushirikino na Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Mauritania.

Waziri wa Masuala ya Kiislamu Saudia Sheikh Abdullatif Al Al-Sheikh amesema mashindano hayo yatafanyika robo ya kwanza yam waka 1444 Hijria Qamaria. Aidha amebaini kuwa lengo la mashindano hayo ni kuimarisha uhusianoa na ushirikiano katika sekta zote kwa maslahi ya Uislamu na Waislamu.

Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ni nchi iliyo katika eneo la Maghreb magharibi-kaskazini mwa Afrika.

Idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa ni milioni nne na karibu Wamauritania wote ni Waislamu. Harakati za Qur’ani ni mashuhuri katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

3479243

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :