IQNA

Msikiti Marekani waharibiwa kwa moto katika hujuma

21:36 - October 13, 2021
Habari ID: 3474420
TEHRAN (IQNA)- Moto ambao unashukiwa kuanzishwa na wenye chuki dhidi ya Uislamu umeharibu jengo la msikiti eneo la University Place, jimboni Washington nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa moto uliibuka katika Msikiti wa Kituo cha Kiislamu cha Tacoma juzi kabla ya kuanza Sala ya Ishaa.

Watu wachache waliokuwa ndani ya msikiti walifanikiwa kuondoka kabla ya moto kuenea na hakuna mtu aliyejeruhiwa. Walioshuhudia wanasema waliona mtu anayeaminika kuwasha moto huo akitoroka eneo la tukio.

Imam wa Msikiti wa Kituo cha Kiislamu cha Tacoma  Sheikh Abdulhakim Mohammad anasema waumini katika msikiti huo wameshtushwa na kitendo hicho na kwamba jengo la msikiti limeharibiwa vibaya sana na kwa sasa haliwezi kutumika. Huo ndio msikiti pekee katika eneo hilo na msikiti ulio karibu uko mbali na waumini watalazimika kusafiri kwa gari kwa muda wa dakika 40 jambo ambalo litakuwa vigumu kwa wengi.

Hivi karibuni uchunguzi mpya umebaini kuwa zaidi ya asilimia 67.5 ya Waislamu wanaoishi Marekani wamekumbana na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu (Islampohobia) walau mara moja maishani.

Halikadhalika asilimia 93.7 ya Waislamu Marekani wanasema vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu huathiri hisia zao na afya ya kiakili.

Uchunguzi huo umefanyika miongo miwili baada ya hujuma za Septemba 11 nchini Marekani ambazo zilisbabaisha ongezeko kubwa  vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu ambavyo vimewalenga mamillioni ya Waislamu Marekani.

3476027

Kishikizo: marekani ، waislamu ، msikiti
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha