IQNA

Msikiti wa karne moja unawakilisha utambulisho uliojaa utata wa Waislamu wa Marekani

11:12 - August 24, 2025
Habari ID: 3481128
IQNA – Huko Cedar Rapids, Iowa, msikiti wa mkongwe zaidi nchini Marekani, ambao ni jengo dogo jeupe la mbao, ni ushahidi wa kimya wa historia ndefu ya Waislamu wa Marekani.

Sasa, huku mizozo ya kigeni ikichochea mivutano ya ndani, vizazi vya waanzilishi wake waliotokea Lebanon na wahamiaji wapya kutoka kila kona ya dunia ya Kiislamu wanajumuika tena kuunda tafsiri mpya ya maana ya kuwa Muislamu kamili na Mmarekani kamili katika moyo wa taifa.

Akisimama kando ya mlango akiwa amevaa vazi la buluu lenye mapambo ya dhahabu, Fatima Igram Smejkal alikaribisha waumini kwa salamu ya furaha ya “Asalaam Aleikum” wakati walipoingia kwa haraka kwenye Kituo cha Kiislamu cha Cedar Rapids kwa sala ya Ijumaa. Mnamo mwaka 1934, familia yake ilisaidia kufungua kile ambacho Orodha ya Kitaifa ya Maeneo ya Kihistoria inakiita “jengo la kwanza lililoundwa na kujengwa mahsusi kama nyumba ya ibada kwa Waislamu nchini Marekani.”

“Wote walikuja eneo ambalo hawakua na chochote ... hivyo walitaka kusaidia,” alisema Smejkal kuhusu familia kama yake, ambazo zilifika mwanzoni mwa karne ya 20. “Hiyo ndiyo sababu mimi ni mkarimu kwa wale wanaokuja kutoka Somalia, Congo, Sudan na Afghanistan. Sina wazo la kile walichokiona, wanachofikiria wanapokuwa wanatembea kuingia kwenye msikiti huo ambao unajulikana kama Mother Mosque.”

Jamii sasa hukusanyika katika Kituo cha Kiislamu. Kiliijengwa katika miaka ya 1970 wakati idadi ilipoongezeka na hivyo kutoweza kutoshea katika Msikiti na sasa idadi pia imeongezeka zaidi.

Mamia ya Waislamu wa kizazi cha tano wa Iowa, wakimbizi na wahamiaji wapya hufanya ibada kwenye zulia kwenye uwanja wa mpira wa kikapu, wazee wakiwa wanatembea kwa fimbo, watoto wakiwa kwenye viti maalumu, wanawake wakiwa na hijabu na wanaume wakiwa na kofia kutoka Afrika na Waafghani wakiwa wamevalia kofia zao za jadi huku vijana wakiwa wamevalia kofia za baseball.

Hii ni nafasi ambayo makundi tofauti hukutana, ikisaidia kudumisha jamii wakati wahamiaji wanajaribu kuhifadhi urithi wao wakati wakichangamana na utamaduni na jamii ya Marekani.

“Unaweza kuwa Muislamu unayefanya ibada yako na bado kuishi kwa amani na kila mtu aliye karibu nawe,” alisema Hassan Igram, ambaye anaongoza bodi ya wadhamini wa kituo hicho. Anashirikiana majina ya kwanza na ya mwisho na babu yake na babu wa Smejkal – binamu wawili waliokuja Iowa wakiwa wavulana katika miaka ya 1910.

Wahamiaji hao  walifanya kazi kuuza bidhaa za nyumbani kutoka kwa mabegi yao kwa mashamba yaliyo mbali, wakipata pesa za kutosha kununua farasi na magari, kisha walifungua maduka ya vyakula.

Kupitia mauzo ya mikate na milo ya jamii, kundi la wanawake Waislamu lilikusanya fedha katika miaka ya 1920 kujenga kile kilichoitwa “Hekalu la Kiislamu.” Kama familia ya Igram, Anace Aossey anakumbuka kuhudhuria sala eneo hilo na wazazi wake.

Kukua Kama Muislamu Nchini Marekani

Waislamu walikumbana na ubaguzi wa taasisi mara kwa mara. Baada ya kuhudumu katika Vita vya Pili vya Dunia, baba wa Smejkal, Abdallah Igram, alifanikiwa kupigania kutambuliwa haki za Waislamu.

Abdallah Igram amezikwa kwenye makaburi ya Waislamu kwenye kilima cha jiji,

Kuwa Muislamu Katika Moyo wa Taifa

Uwepo wa Waislamu katika eneo la Midwest uliongezeka kwa kasi baada ya sheria ya uhamiaji ya mwaka 1965 kuondoa masharti ambayo yalizuia wahamiaji kutoka sehemu nyingi za dunia tangu katikati ya miaka ya 1920.

Ubaguzi ulizuka tena baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001, hasa katika jamii za kilimo ambapo vijana wao walikuwa wakipigana huko Afghanistan na Iraq, alisema Ako Abdul-Samad, Mmarekani Mweusi aliyeiwakilisha Des Moines kwa takriban miongo miwili katika Bunge la Jimbo la Iowa. Alikuwa na hofu kwamba kuwa Muislamu kutazuia kuchaguliwa kwake alipokuwa anagombea ofisi, lakini wapiga kura walimchagua tena na tena.

Uhamiaji, ikiwa ni pamoja na kutoka nchi za Kiislamu, bado ni suala linalozua mjadala, ingawa jamii za Kiislamu zinastawi na kuongezeka kwa ushawishi wao wa kisiasa katika miji mikubwa kama Minneapolis na Detroit.

Lakini mwingiliano wa kila siku kati ya Waislamu na majirani zao umeleta ulinzi kutoka kwa ubaguzi, kulingana na imam wa Msikiti wa Mother Mosque, Mpalestina aliyehamia eneo hilo katika miaka ya 1980. “Mifano ya kutengwa haikutumika” Cedar Rapids, alisema Taha Tawil.

Waislamu wa Kibosnia wanasema walikumbana na uzoefu kama huo karibu na Des Moines, ambapo msikiti mpya wa mamilioni ya dola na kituo cha kitamaduni kitafunguliwa mwezi ujao, ni upanuzi wa kituo cha kwanza kilichojengwa na wakimbizi wa vita miaka 20 iliyopita.

Kuwa Wa Midwest

Faroz Waziri anacheka kwamba yeye na mkewe Mena pengine walikuwa Waislamu wa kwanza kutoka Afghanistan walipoingia mji huu katikati ya miaka ya 2010 kwa visa maalum kwa wale waliowahi kufanya kazi kwa vikosi vya kijeshi vya Marekani nje ya nchi. Baada ya kupambana na “mshtuko wa utamaduni” na vizuizi vya lugha, wamekuwa raia wa Marekani.

“Kihisia na kiakili, sidhani kamwe kuwa mimi ni Mmarekani,” anasema Mena Waziri. Yeye ni mhitimu wa chuo na anapenda uhuru na haki za wanawake ambazo bado ni vigumu kufikiwa nchini Afghanistan inayoongozwa na Taliban. Lakini familia inataka mtoto wao aliyezaliwa Marekani, Rayan, kuwa na marafiki wa Kiislamu na maadili ya Kiislamu.

3494366

captcha