IQNA

EU yakosoa hatua ya Israel kujenga vitongoji zaidi vya walowezi mjini Quds

21:57 - October 29, 2021
Habari ID: 3474486
TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Ulaya (EU) umekariri wito wake kwa utawala haramu wa Israel usitishe mpango wake wa kujenga vitongoji zaidi vya walowezi wa Kizayuni katika mji wa Quds (Jerusalem).

Katika taarifa Ijumaa, Mkuu wa Sera za Kigeni katikak Umoja wa Ulaya Josep Borrell  ametahadharisha umoja huo hautatmabua mabadiliko yoyote katika mipaka ya kabla ya 1967 na kuongeza kuwa: "Vitongoji ni kinyume cha sheria kwa mujibu wa kanuni za kimataifa na kizingiti cha kufikia amaani ya kudumu baina ya pande mbili."

Siku ya Jumatano utawala ghasibu wa Israel ulitangaza kujenga vitongoji mpya 3,000 vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Kwa muda mrefu sasa utawala wa Kizayuni umekuwa ukiteka ardhi za Wapalestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwa lengo la kuvuruga muundo wa kijiografia na kijamii katika maeneo ya Wapalestina kwa uungaji mkono wa kila upande wa Marekani.

Utawala wa Kizayuni unaendeleza ujenzi huo haramu wa vitongoji katika ardhi za Palestina huku ukipuuza takwa la jamii ya kimataifa la kusimamisha ujenzi huo kwa kukingiwa kifua na Marekani. Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, ujenzi wa vitongoji vyote vya walowezi wa Kizayuni unaofanywa na Israel katika ardhi za Palestina ni kinyume cha sheria.  

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, hadi sasa utawala wa Israel haujachukua hatua yoyote ya kutekeleza azimio nambari 2234 la tarehe 23 Disemba 2016 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 

4008734

captcha