IQNA

Walowezi wa Kizayuni wauhujumi Msikiti wa Al Aqsa

21:15 - November 01, 2021
Habari ID: 3474499
TEHRAN (IQNA)- Walowezi za Kizayuni wameendeleza hujuma zao dhidi ya msikiti wa Al Aqsa katika mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem).

TEHRAN (IQNA)-  Walowezi za Kizayuni wameendeleza hujuma zao dhidi ya msikiti wa Al Aqsa katika mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem).

Kwa mujibu wa mashuhuda, walowezi hao wa Kizayuni wenye misimamo mikali wametekeleza hujuma hiyo chini ya ulinzi mkali wa  jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel.

Walowezi wao waliingia katika msikiti huo kupitia lango la Al Magharibah na kisha kutekeleza ibada zao za Kizayuni ndani ya uwanja wa eneo hilo takatifu la Kiislamu.

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, wakuu wa nchi za Kiarabu na viongozi wa kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

3476297

captcha