IQNA

Utawala haramu wa Israel kujenga nyumba 3000 katika ardhi zilizoporwa mjini Quds

15:27 - November 25, 2021
Habari ID: 3474597
TEHRAN (IQNA)- Utawala haramu wa Israel umeidhinisha ujenzi haramu wa nyumba 3000 za walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina zilizoghusubiwa na kukoloniwa na utawala huo katika mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem)

Idhini hiyo ilitolewa Jumatano na manispaa maalumu iliyoteuliwa na watawala wa Tel Aviv kwa ajili wa ujenzi wa nyumba hizo katika eneo ambalo zamani lilikuwa uwanja wa ndege karibu na mji wa Ramallah katika Ukingo wa Magharibi wa Mti Jordan.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP, mradi wa ujenzi wa nyumba hizo utatekelezwa katika hatua kadhaa ambapo katika hatua ya baadaye nyumba nyingine 6000 zitaongezwa katika mradi huo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Ndani ya Plaestina imekosoa vikali mradi huo haramu wa ujenzi wa nyumba za walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina zilizoghusubiwa na kuitaka jamii ya kimataifa iingilie kati ili kuulazimisha utawala haramu wa Isreal usimamishe mara moja ujenzi wa nyumba hizo.

Utawala haramu wa Israel ulikalia kwa mabavu ardhi za magharibi mwa mji mtakatifu wa Quds ambazo zinajumuisha Msikiti wa al-Aqsa ambao ni msikiti wa tatu kwa utukufu katika ulimwengu wa Kiislamu mwaka 1948. Mwaka 1967 ulikalia kimabavu ardhi zaidi za mashariki ambazo Malaka ya Ndani ya Palestina imedhamiria kuzifanya kuwa mji mkuu wake.

Licha ya kuwa jamii ya kimataifa inazochukulia ardhi hizo kuwa zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa kibaguzi wa Israel lakini haijachukua hatua zozote za maana za kuulazimisha utawala huo uwarudishie Wapalestian ardhi zao hizo.

3476647

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha