IQNA

Maelfu washiriki katika Maulid ya Mtume Muhammad SAW Lamu, Kenya

18:06 - November 03, 2021
Habari ID: 3474508
TEHRAN (IQNA)- -Maelfu ya watu kutoka kote duniani wamehudhuria sherehe za Maulid ya Mtume Muhammad SAW ambazo zimefanyika katika Kisiwa cha Lamu eneo la Pwani ya Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa mwaka huu wageni 6,000 wanahudhuria sherehe za wiki nzima za kukumbuka kuzaliwa Mtume Muhammad SAW yaani Miladun Nabii ambazo mwaka hii ni za 134.

Sherehe hizo ambazo ni za aina yake zinafanyika katika Msikiti maarufu wa Riyadha katika kisiwa cha Lamu.

Msikiti wa Riyadha ni kati ya misikiti iliyotumika kwa muda mrefu zaidi katika ukanda wa mwambao wa Afrika Mashariki na ni kitovu cha kmafunzo ya Kiislamu.

Akizungumza na waandishi habari, Katibu Mkuu wa Msikiti wa Riyadha Abubakr Mohamma Badawyi amesema mwaka huu kuna wageni kutoka nchi kama vile Morocco, Visiwa vya Comoro nan chi zote jirani. Halikadhalika kutokuwa na washiriki kutoka maeneo yote ya Kenya.

Sherehe za mwaka hii zinatumika pia kutoa mafunzi kuhusu umuhimu wa watu kuishi kwa umoja na amani wakati huu ambapo Kenya inaitayarisha kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Wakazi wa Lamu na wageni wanaoshiriki katika Maulidi mwaka huu watapata matibabu kutoka kwa madaktari na wataalmu 45 waliofika kisiwani hapo kutoka Mombasa na Nairobi.

Kati ya matibabu watakayopata ni kupimwa saratani, upasuaji wa macho, vipimo vya shinikizo la damu n.k. Aidha Maulid ya mwaka huu pia itajumuisha mashindano ya kuoglekea, mashindano ya mashua, kaligrafia ya Kiislamu na Zefe.

Kilele cha Maulidi ya mwaka huu Lamu ni Alhamisi na Ijumaa washiriki wa mashindano wanatazmiwa kutunukiwa zawadi katika Msikiti na Kituo cha Kiislamu cha Riyadha.

Mji wa Lamu ni kati ya miji ya kale zaidi katika mwambao wa Afrika Mashariki na ni turathi muhimu ya Uislamu na ustaarabu wa Waswahili.

/3476327

captcha