IQNA

Maulid ya Mtume Muhammad SAW

Sherehe za Milad-un-Nabi zafanyika katika misikiti ya Istanbul, Uturuki

17:38 - October 08, 2022
Habari ID: 3475897
TEHRAN (IQNA) – Misikiti katika mji wa Uturuki wa Istanbul imeandaa sherehe za Milad-Un-Nabi za kukumbuka kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW).

Idadi kubwa ya Waislamu maashiqi wa Mtume Muhammad SAW walihudhuria sherehe hizo kwenye misikiti katika mji mkubwa wa Uturuki siku ya Ijumaa.

Sherehe hizo zilijumuisha usomaji wa Qur'ani Tukufu, hotuba za kidini zilizotolewa na maulama wa Kiislamu, usomaji wa dua na qasida za kumsifu Mtume Muhammad SAW.

Msikiti wa Sultan Ahmed (pia unajulikana kama Msikiti wa buluu), Msikiti wa Suleymaniye, Msikiti wa Fatih na Msikiti wa Camlica ni miongoni mwa walioandaa hafla hizo.

Watu waliohudhuria sherehe za Msikiti wa Fatih walipokea zawadi kutoka kwa manispaa ya Wilaya ya Fatih baada ya kuondoka msikitini.

Kulikuwa na sherehe kama hizo zilizoandaliwa katika miji katika maeneo mengine ya Uturuki.

Uturuki ni nchi yenye Waislamu wengi katika  eneo la Asia Magharibi. Takriban asilimia 99 ya wakazi wa nchi hiyo wanafuata Uislamu.

Jumapili, Oktoba 9, ni siku ya 12 Mfunguo Sita Rabi al-Awwal, ambayo, kwa mujibu wa Waislamu wa Sunni, ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW). Waislamu wa madhehebu ya Shia duniani kote husherehekea hafla hiyo nzuri siku ya 17 ya mwezi (ambayo ni Ijumaa, Oktoba 14 mwaka huu).

Milad-un-Nabi Celebrations Held at Istanbul Mosques

Milad-un-Nabi Celebrations Held at Istanbul Mosques

Milad-un-Nabi Celebrations Held at Istanbul Mosques

4090222

captcha