IQNA

Milad un Nabii

Algeria Inajiandaa Kuadhimisha Maulid ya Mtume Muhammad (SAW) na Wiki Qur'ani Tukufu

22:12 - September 26, 2023
Habari ID: 3477658
ALGIERS (IQNA) - Waziri Wakfu na Masuala Kidini wa Algeria katika kikao na wasimamizi wa wizara hiyo walijadili kufanya sherehe za kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) yaani Maulidi au Milad un Nabii.

Pia walizungumza kuhusu maandalizi ya Wiki ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu nchini humo, ambayo itakuwa toleo la saa 25 la mwaka huu.

Youcef Belmehdi, Waziri wa Wakfu, aliwaamuru maafisa husika kuhakikisha sherehe na hafla ya Qur'ani inapangwa kwa njia bora zaidi.

Vile vile alitoa amri ya kuwaheshimu wahifadhi Qur'ani na washairi mahiri wakati wa sherehe hizo.

Toleo la 25 la wiki ya kitaifa ya Qur'ani ya Algeria litajumuisha mashindano ya Qur'ani, ambayo duru yake ya awali tayari imeanza.

Zaidi ya washindani 200 hushindana katika kategoria za kuhifadhi Qur'ani, usomaji na Tafseer (tafsiri) wakati wa kipindi cha Milad un Nabii.

Pia kuna mashindano tofauti kwa wanawake katika kategoria ya kuhifadhi Quran.

Kila mwaka, Waislamu kote ulimwenguni hufanya sherehe na programu mbalimbali katika mwezi wa Rabi al-Awwal (ulioanza Septemba 17) kusherehekea ukumbusho wa kuzaliwa kwa mjumbe wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, Muhammad Al Mustafa (SAW).

 

4171251

Habari zinazohusiana
captcha