IQNA

23:00 - January 15, 2022
Habari ID: 3474808
TEHRAN (IQNA)- Duru ya Saba ya Mashindano ya Kimataifa ya Wanafunzi wa Shule itafanyika Iran kwa kushiriki wawakilishi wan chi 25.

Mikael Bagheri, Mkurugenzi Mkuu wa Qur’ani, Etrat na Sala katika Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu ya Iran ameyasema hayo mjini Tehran alipotembelea makao makuu mashindano hayo.

Nchi ambazo zitashiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Iran, Uturuki, Tanzania, Nigeria, Indonesia, Lebanon, Afghanistan, Iraq, Senegal, Congo, Bangladesh, Ujerumani, Uholanzi, Algeria, Syria, Ivory Coast, Moldova, Pakistan, Sweden, Sri Lanka, Bosnia na Herzegovina, India, Kyrgyzstan, Brunei na Madagascar.

Bagheri amesema majaji wa mashindano hayo watakuwa ni kutoka Iran na nchi kadhaa ambapo sehemu kubwa ya mashindano hayo itafanyika kwa njia ya intaneti.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanafunzi wa Shule hufanyika kila miaka miwili nchini Iran lakini mwaka jana yaliakhirishwa kutokana na janga la corona.

Fainali ya mashindano hayo inatazamiwa kufanyika baina ya Februari na Machi sambamba na mashindano ya kila mwaka ya kimataifa ya Qur’ani ya Iran.

1400102517927

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: