IQNA

Mtaalamu wa Jordan aipongeza Iran kwa kuandaa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani

21:13 - March 04, 2022
Habari ID: 3475006
TEHRAN (IQNA) – Mtaalamu wa Qur'ani Tukufu wa Jordan ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kutositisha mashindano yake ya kimataifa ya Qur'ani pamoja na kuwepo janga la corona.

Samih Ahmed Khalid al-Athamina, ambaye anahudumu katika jopo la majaji wa Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran, alisema nukta hiyo inaonyesha jinsi ilivyo muhimu kuandaa mashindano hayo katika hali yoyote.

Alisema kwa kuzingatia kuwa karibu watu wote wanaweza kupata huduma za intaneti na hivi sasa kufanya kazi kupitia mtandao wa intaneti ni jambo la kawaida, hakuna sababu ya kutoandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kupitia mtandao wa intaneti kwa vile janga hilo limeweka vikwazo kwa shughuli za ana kwa ana.

Alitaja mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran kama "mama wa mashindano wa Qur'ani."

Athamina alisema hajaona ukamilifu kama huu katika mashindano ya Qur'ani ya nchi nyingine, akibainisha kuwa Iran hivi sasa kunafanyika wakati moja mashindano ya kimatiafa ya Qur’ani kwa ajili ya wanaume, wanawake, wanafunzi wa shule na wenye ulemavu wa macho.

Vile vile ameashiria uwepo wa idadi kubwa ya wataalamu wa Qur'ani katika jopo la majaji katika hafla ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran.

Awamu ya mwisho ya mashindano ya 38 ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran ilianza katika sherehe mjini Tehran siku ya Jumatatu na washindi watatangazwa katika hafla ya kufunga Jumamosi.

Jumla ya makari 62 na wahifadhi kutoka nchi 29 wanashindana katika hatua hii ya hafla hiyo, ambayo inafanyika karibu.

Sambamba na hilo, shindano la 5 la kimataifa la Qur'ani kwa wenye ulemavu wa macho, shindano la 7 la kimataifa la Qur'ani kwa wanafunzi wa shule, na mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa wanawake pia yanafanyika, kwa hakika.

Kwingineko katika matamshi yake Athamina alibainisha kuwa amesafiri nchini Iran mara 13 kuhudumu kama mjumbe wa jopo la majaji katika mashindano tofauti ya kimataifa ya Qur'ani.

Amebainisha kuwa hivi sasa anaongoza jopo la wanazuoni nchini Jordan lililopewa jukumu la kusimamia uchapishaji wa Qur’ani nchini humo.

Pia amesema ana watoto watatu wa kiume na wa kike wawili ambao wote ni wahifadhi wa Quran.

مسابقات بین المللی قرآن

Iran Int’l Quran Contest

4039990

captcha