IQNA

Matukio ya Palestina

Wazayuni wapanga njama ya hujuma mpya dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa

23:41 - April 07, 2022
Habari ID: 3475097
TEHRAN (IQNA)- Makundi ya Wazayuni wenye misimamo mikali wametoa wito wa kuhujumiwa Msitiki wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) mnamo Aprili 15 sambamba na 14 Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa mnasaba wa siku kuu ya Kiyahudi wa Pasaka.

Taarifa zinadokeza kuwa katika siku hiyo Wazayuni wenye misimamo ya kufurutu ada wakiwa wanapata himya ya jeshi la utawala ghasibu wa Israel  wanalenga kuhujumu eneo hilo la tatu takatifu katika Uislamu. Aidha imearifiwa kuwa Makuhani wa Kiyahudi wanapanga kutekeleza wanapanga kuchinja kondoo katika msikiti huo wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu na hivyo kuvunjia heshima eneo hilo takatifu la Kiislamu.

Umoja wa Mataifa uchukue hatua dhidi ya Israel

Kwingineko, Mkuu wa ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameutaka Umoja wa Matafa utekeleze majukumu yake kwa kuchukua hatua dhidi ya uvamizi na chokochoko za utawala wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Utawala haramu wa Israel umetuma wanajeshi elfu tatu mjini Quds sambamba na kuwadia mwezi Mtukufu wa Ramadhani; ambapo wanajeshi hao hadi sasa wametekeleza mashambulizi kadhaa katika usiku wa tatu mfululizo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani dhidi ya Wapalestina waliokuwa wamekusanyika katika eneo la kihistoria la Bab al Amoud na kuwajeruhi raia kadhaa wa Kipalestina.

Televisheni ya Palestine al Yaum imeripoti kuwa, Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas amezungumza kwa simu na Tor Wennesland Mratibu Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika mchakato wa amani Asia Magharibi kuhusu matukio ya karibuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.  

Katika mazungumzo hayo, Hania ameeleza kuwa Umoja wa Mataifa unapasa kutekeleza majukumu yake ili kuzuia kuendelea uvamizi na mashambulizi ya Wazayuni katika msikiti Mtukufu wa al Aqsa na dhidi ya raia wa Palestina khususan katika wakati huu wa mfungo mtukufu wa Ramadhani. Imeelezwa kuwa, katika siku za karibuni, wakazi wa maeneo yanayokaliwa kwa mbavu ambayo yanajulikana kama ardhi zilizovamiwa na kukaliwa kwa mabavu mwaka 1947; katika ripoti maalumu ya Umoja wa Mataifa wameeleza wazi hali ya maafa inayowakabili.

Kamatakamata ya Wapalestina

Hayo yanajiri wakati ambao, vikosi vya utawala haramu wa Israel vimewashambulia Wapalestina katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuwatia mbaroni 13 miongoni mwao. Shirika la habari la Wafa la Palestina limeripoti hayo leo Alkhamisi na kuongeza kuwa, askari wa utawala wa Kizayuni walifanya operesheni hiyo ya kamatakamata usiku wa kuamkia katika mji wa Ramallah na miji inayopakana nao kama vile al-Bireh.

Habari zaidi zinasema kuwa, Wapalestina wengine wamekamatwa katika mji wa Nablus, baadhi katika kambi ya wakimbizi ya Jalazone kaskazini mwa Ramallah, na wengine katika kambi ya al-Am'ari, kusini mwa mji wa al-Bireh.

Inaarifiwa kuwa, wanajeshi makatili wa Israel walishambulia nyumba za Wapalestina hao waliokuwa na jamaa zao kabla ya kuwakamata kwa mabavu na idhilali.

/4047568

captcha