IQNA

Waislamu Ghana washiriki kikao cha Qur’ani kuomba baraka za Allah SWT

18:25 - January 06, 2022
Habari ID: 3474772
TEHRAN (IQNA) – Waislamu nchini Ghana wameshiriki kikao cha kusoma Qur’ani kwa ajili ya kuomba baraka za Allah SWT.

Kwa mujibu wa taarifa kikao hicho kimeandaliwa na jamii ya Waislamu ya Ayawaso katika mji wa Accra mnamo Januari Mosi ambapo washiriki wamemuomba Allah SWT aijalie Ghana ipata baraza za amani umoja, na ustawi.

Kikao hicho cha kwanza cha aina yake kimeitishwa na Sheikh Mustafa Yaajala, imamu wa Msikiti wa Markaz Al Mihi katika mtaa wa Kanda 441.

Waislamu hao walihitimisha Qur’ani mara tatu katika kikao hicho na baada ya hapo wakachinja ngo’ombe huku wakiwaombea afya watu wote na maghfira kwa waliotangulia mbele ya haki.

Walioshiriki katika kikao hicho wamehimizwa kuafiki kudungwa chanjo ya COVID-19 ili kuzuia kuenea kirusi hicho huku wakitakiwa kuzingatia kanuni za kiafya kama vile kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa sabuni mara kwa mara na kutokaribiana katika mijiumuiko mikubwa.

/3477257

Kishikizo: ghana waislamu
captcha