IQNA

Mashindano ya Qur’ani ya Mauritania kuwa na washiriki 2,000

21:37 - March 14, 2022
Habari ID: 3475040
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani nchini Mauritania yatafanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa, mashindano hayo yanatazamiwa kuwa na washiri 2,000 katika duru ya awali ya mchujo.

Jopo la majaji litajumuisha  kamati nne za kitaalamu ambazo zinawalet pamoja wataalamu wa Qur’an Tukufu na Maqarii.

Finali ya mashindano hayo inatazamiwa kuanza katika siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo washiriki bora 63 watatunikiwa zawadi baada ya kumalizika mashindano.

Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritani ni nchi iliyo katika eneo la Maghreb magharibi-kaskazini mwa Afrika.

Idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa ni milioni nne na karibu Wamauritania wote ni Waislamu. Harakati za Qur’ani ni mashuhuri katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

4042218

captcha