IQNA

Harakati za Qur'ani

Jumuiya ya Walimu wa Qur'ani yaanzishwa nchini Mauritania

11:33 - December 04, 2022
Habari ID: 3476193
TEHRAN (IQNA) - Jumuiya ya walimu na wataalamu wa Qur'ani Tukufu iliyoanzishwa nchini Mauritania ilianza shughuli zake katika sherehe iliyofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nouakchott.

Inalenga kuandaa na kuratibu shughuli za walimu na wataalamu wa Qur'ani na kuboresha hali zao ili kuwahudumia vyema wanafunzi wa Qur'ani, msemaji wa shirika hilo alisema.

Akihutubia kwenye hafla ya ufunguzi, Lamrabit Ould Sayedi alisema kuwa pia inalenga kuondoa vikwazo katika shughuli za walimu.

Alisema wazazi wanaweza kutegemea shirika hilo kuwa chanzo kizuri cha kuchagua walimu wa Qur'ani Tukufu wenye sifa za kitaaluma na kimaadili za kuwafundisha watoto wao.

Jumuiya hiyo linatumika kama kiungo kati ya familia, taasisi za Qur'ani Tukufu na pia walimu na wataalamu wa Qur'ani Tukufu, msemaji huyo aliongeza.

Aliendelea kusema kuwa jumuiya hiyo itajitahidi kukuza kazi ya timu kati ya wanachama wake na kuinua kiwango cha ujuzi na ustadi wao.

Lamrabit Ould Sayedi pia alisoma aya za Qur'ani Tukufu katika hafla ya ufunguzi. Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ni nchi iliyoko katika eneo la Maghreb magharibi mwa Afrika Kaskazini.

Idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa takriban milioni 4 na takriban Wamauritania wote ni Waislamu. Shughuli na programu za Qur'ani Tukufu ni maarufu sana katika nchi ya Kiafrika.

Ifuatayo ni klipu ya usomaji wa Qur'ani wa Lamrabit Ould Sayedi:

4104096

captcha