IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Adui amefanya makosa katika hesabu zake, taifa la Iran limechagua mantiki ya Mapinduzi ya Kiislamu

16:32 - March 17, 2023
Habari ID: 3476717
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya wiki hii mjini Tehran amesisitiza kuwa: adui amefanya makosa katika hesabu zake huku taifa la Iran likichagua mantikiya Mapinduzi ya Kiislamu.

Hujjat-ul-Islam wal-Muslimeen Mohammad Javad Haj Ali Akbari aliyasema hayo katika khutba za Sala ya Ijumaa ya Tehran na kuongeza kuwa: "Operesheni kali ya zaidi ya siku 100 iliiweka nchi hatarini na  mashinikizo ya pande zote ili kuvuruga mafanikio yaliyofikiwa katika meza ya mazungumzo lakini  taifa lilisimama dhidi ya fitina tatu kubwa katika msimu uliopita wa vuli."

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya wiki hii mjini Tehran ameongeza kuwa maadui waliingia katika medani kwa kutekeleza mauaji kwa njia isiyo ya kawaida.

Haj Ali Akbari pia alisema: Waliendelea na mpango wao kwa kuwatia sumu wanafunzi na kutoa wito wa ghasia katika Jumatano ya mwisho wa mwaka wa 1401 Hijria Shamsia sambamba na diplomasia ya kishetani iliyokuwa na lengo la kuitenga Iran kwa kisingizio cha haki za binadamu.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran ameendelea kusema kuwa: "Ingawa mipango ya maadui ilikuwa sahihi, lakini walikuwa wamefanya makosa katika hesabu zao na hawakuwa na ujuzi wowote kuhusu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu."

Haj Ali Akbari amesisitiza kuwa mfumo wa Kiislamu uliweza kuonyesha huruma kupitia msahama wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa wale waliodanganywa na kujihusisha katika ghasia zilizokuwa zimeikumba baadhi ya miji ya Iran katika miezi ya hivi karibuni.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya wiki hii mjini Tehran ameongeza kuwa: Hali ya mapambano au muqawama katika mwaka wa Kiirani wa 1401 Hijria Shamsia unaokaribia kumalizika ilikuwa nzuri sana kwani Syria imerudi katika Jumuiya ya Nchi za  Kiarabu, Iraq imeunda serikali mpya, Palestina  imetoa pigo kali kwa utawala wa Kizayuni, Lebanon imesimama kidete dhidi ya njama za maadui Wazyauni na waitifaki wao katika nchi za Kiarabu. Amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unawaua watoto ndio uliopata hasara kubwa katika matukio hayo yote.

Haj Ali Akbari alisema kuwa hali si nzuri barani Ulaya na kusema: "Vita vya Ukraine vimeathiri zaidi uhusiano na mwelekeo wa kimataifa na vimeanzisha mgogoro katika uchumi wa magharibi na uchumi wa kimataifa." Aidha amesema watawala wa Mareani ni  wajinga na hawataweza kuwa na busara na ujinga wao unaendelea.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran pia amesema: Marekani imekabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi katika kipindi cha mwaka moja uliopita na hali yake ya kijamii hivi sasa si nzuri huku ikiendelea kukumbwa na janga la corona.

4128634

captcha