IQNA

Kimbunga cha Al-Aqsa

Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Siku ya Kimbunga cha Al-Aqsa ni siku ya baraka kwa watu wa Palestina

20:29 - October 27, 2023
Habari ID: 3477794
TEHRAN (IQNA) - Akizungumzia mafanikio ya operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesema: "Siku ya (Kimbunga) Tufani ya Al-Aqsa" inapaswa kuzingatiwa kuwa Siku ya Al Baraka kwa watu wa Palestina na Siku ya Nakba kwa utawala wa Kizayuni.

Hujjatul Islam "Mohammed Javad Haj Ali Akbari", khatibu wa Swala ya Ijumaa wiki hii jijini Tehran katika hotuba yake ameeleza kuwa mada muhimu zaidi siku hizi ni kadhia ya Palestina na kuongeza kuwa: "Kimbunga cha al Aqsa" ni operesheni kubwa iliyoambatana na mabadiliko ya kihistoria ambapo historia ya eneo na ulimwengu inapaswa kugawanywa kabla na baada ya Oktoba 7 2023.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa amesema: "Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ni jibu la miaka 75 la kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina na mzingiro wa miaka 16 wa Ukanda wa Ghaza." Amesema operesheni hiyo ni dhidi ya lobi au makundi ya mashinikizo ya kimataifa ya Wazayuni, Marekani na Ulaya. Aidha amesema msingi na utambulisho wa lobi hiyo ni mauaji, kudhalilisha wengine na kuharibu maisha ya binadamu.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa jijini Tehran ameashiria kwamba sura halisi ya demokrasia ya kiliberali ya Magharibi imedhihirika katika matukio ya hivi karibuni huko Ghaza na kusema: "Dunia nzima imeona namna ambayvo hivi karibuni watawala wa Marekani na Ulaya walifika katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) wakiwa wamejaa hofu, lakini ifahamike kuwa utawala wa Kizayuni ambao ni sawa na uvimbe wa saratani ambao utapelekea kuangamia kwake, ulipata pigo kubwa katika uti wa mgongo wake katika operesheni ya hivi kaibuni na hauwezi tena kusimama."

Inafaa kuashiria hapa kuwa katika kukabiliana na jinai za Wazayuni, vikosi vya muqawama vya Palestina vilianza operesheni ya "Tufani ya Al Aqsa" ukanda wa Ghaza dhidi ya ngome za utawala wa Kizayuni  wa Israel kuanzia Jumamosi, Oktoba 7, 2023.

Tangu kuanza kwa operesheni hiyo, jeshi la Kizayuni, ambalo halina uwezo wa kukabiliana na wapiganaji wa muqawama, limekuwa likishambulia kwa mabomu maeneo ya raia, hospitali, vituo vya kidini na shule huko Ghaza.

Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Afya ya Palestina, zaidi ya watu 7,800 wameuawa shahidi na wengine takriban 20,000 wamejeruhiwa katika siku 21 za jinai za utawala wa Kizayuni katika ukanda wa Ghaza.

4178101

Habari zinazohusiana
captcha