IQNA

Jinai za Israel

Askari watenda jina wa Israel waua shahidi Wapalestina wawili

20:48 - September 01, 2022
Habari ID: 3475718
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Kizayuni wa Israel umeendeleza jinai na chokochoko zake dhidi ya mataifa mawili ya Waislamu katika eneo hili la Asia Magharibi.

Wanajeshi makatili wa utawala huo pandikizi wamewaua shahidi mabarobaro wawili wa kiume wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Kituo cha Habari cha Palestina kimeripoti kuwa, vijana hao wa Kipalestina Yazan Afana na Samer Khaled, wameuawa shahidi baada ya askari wa Israel kuvamia kitongoji cha Umm Al Sharayet katika eneo la Al-Bireh, na kuibua makabiliano baina ya wakazi wa eneo hilo la Ukingo wa Magharibi na vikosi vya Kizayuni.

Aidha vikosi hivyo vya Israel vimeshambulia kambi ya wakimbizi ya Balata mashariki mwa mji wa Nablus, na kusababisha kuibuka mapigano baina ya wakazi wa eneo hilo na askari wa utawala huo haramu. 

Kwingineko,utawala khabithi wa Israel umefanya mashambulio kadhaa dhidi ya Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Allepo (halab), magharibi mwa Syria.

Shirika rasmi la habari la Syria SANA limeripoti hayo na kueleza kuwa, Tel Aviv imeshambulia kwa makombora kadhaa uwanja huo na kuharibu suhula na miundomsingi yake.

Ripoti ya shirika la SANA haijabainisha iwapo kuna watu wameuawa au kujeruhiwa kwenye hujuma hiyo ya Wazayuni mjini Halab usiku wa kumkia leo.  

4082414

Habari zinazohusiana
captcha