IQNA

Milango ya Msikiti huko Melbourne imefunguliwa kwa kila mtu

22:23 - March 14, 2022
Habari ID: 3475043
TEHRAN (IQNA) – Baada ya masaa mengi ya kuchangisha fedha, kupanga na kujenga, milango ya msikiti mpya kabisa huko Melbourne, Australia, hatimaye imefunguliwa.

Mradi huu ulianza kama ndoto ya jamii zaidi ya muongo mmoja uliopita.

Msikiti Mkuu wa Melbourne huko Tarneit, utahudumia watu wa tamaduni mbali mbali katika eneo hilo.

Katika muda wa muongo mmoja, pedi katika baraza la Wyndham zimebadilishwa kuwa vitongoji vipya ambavyo vinaanza kukuza tabia zao tofauti.

Msikiti huo ambao umegharimu dola milioni 8.5 na ujenzi huo umegharimiwa kwa misaada ya watau wa jamii hiyo bila kutegemea misaada ya kigeni.

Baada ya msikiti pia kuna mipango ya ujenzi wa ukumbi wa jamii na kituo cha michezo kujengwa.

"Kila mtu anakumbatiana na anaonyesha furaha yake," Raheem alisema.

"Huu ulikuwa mradi ambao ulianza mwaka wa 2008 ... Katika mafanikio yote katika maisha yangu, haya ndiyo mafanikio bora zaidi niliyopata."

Wengi, kama baba wa watoto wanne Ibrahima Diouf, walihamia eneo hilo ili tu kuwa karibu na msikiti na shule ya Kiislamu iliyo kando ya barabara.

"Ni muhimu sana kuunganishwa na kuweza kuwa na eneo kama hili," alisema.

Wale wanaoendesha msikiti wanasema wanataka kuwakaribisha watu kutoka tabaka zote za maisha - na imani.

Sheikh Saeed Warsama Bulhan alikuwa alikuwa mwenye tabasamu Jumapili wakati mamia ya watu wakimiminika kwenye Msikiti Mkuu wa Melbourne kwa siku yake ya kwanza ya wazi.

Imam mwenye umri wa miaka 37 alikuwa na shughuli nyingi akiwakaribisha wageni na kuzungumza juu ya matarajio yake.

"Tutakuwa na matukio ya ustawi, tutakuwa na ushauri nasaha, tutakuwa na elimu, tutakuwa na shughuli na maeneo ya kucheza kwa vijana na watoto," alisema.

"Sio msikiti wa Waislamu tu, sio msikiti wa wazee tu, sio msikiti wa kundi moja la jamii. Huu ni msikiti wa kila mtu."

Misikiti mingi katika nchi za Magharibi huwa na mpango wa kuwakaribisha wasiokuwa Waislamu katika nyakati maalumu ili wajifunze Uislamu kutoka kwa Waislamu badala ya kutegemea vyombo vya habari ambavyo hupotosha ukweli kwa makusudi ili kuzuia Uislamu kuenea zaidi.

3478161

captcha