IQNA

Hijabu katika Uislamu

Seneta Muislamu Australia asema atarekebisha mtazamo kuhusu Hijabu

10:37 - June 25, 2022
Habari ID: 3475422
TEHRAN (IQNA) – Fatima Payman, ambaye amechaguliwa kuwa mwanamke wa kwanza wa Muislamu aliyevalia hijabu katika Bunge la Seneti nchini Australia, anasema anataka kuhakikisha kuwa uvaaji

Muislamu wa Australia mwenye umri wa miaka 27, aliyethibitishwa kuwa seneta mpya zaidi wa chama cha Leba kutoka Australia Magharibi akizungumza Juni 13, alisema atavaa Hijabu kwa fahari.

"Nataka kuhakikisha uvaaji wa Hijabu ni jambi la kawaida," Payman aliambia gazeti la Guardian Australia.

“Natumaini kuwa msukumo kwa vijana wengine wengi wa Australia, kwamba kwa sababu tu umamuamini Mwenyezi Mungu, au kwa sababu tu unaonekana tofauti, haipaswi kukuzuia kuhusika katika taasisi muhimu.

Kisa kifupi kuhusu jinsi Payman alifika alipo

Alikuwa na umri wa miaka mitano tu alipokimbia Afghanistan na familia yake, akitafuta hifadhi baada ya Taliban kunyakua madaraka. Familia yake ililengwa kwa sababu babu yake alikuwa mbunge wa Afghanistan.

Kutoka Pakistani, babake, Abdul Wakil Payman, aliondoka kwa boti hadi Australia, "kutafuta maisha bora kwa watoto wake".

Miaka mitatu baadaye, Payman, mama yake na kaka zake walijiunga naye huko Perth, ambapo alifanya kazi tatu - kama msaidizi jikoni, mlinzi na dereva wa teksi. Mama yake aliendesha biashara ya kutoa masomo ya udereva.

Payman alisema baba yake "kila mara alizungumza kuhusu siasa" baada ya chakula cha jioni, akitumaini kwamba siku moja anaweza kurudi Afghanistan ili kuchaguliwa katika bunge la nchi yake.

"Hakuwaza kamwe kuwa na wazo kwamba siku moja binti yake ataweza kuwania useneta  nchini Australia," asema.

Baada ya baba yake kufariki kutokana na saratani ya damu mwaka wa 2018, Payman alijishughulisha na siasa, na kujiunga na Umoja wa Wafanyakazi kama mratibu.

"Nilipojiunga na chama niligundua kuwa ningeweza kupigania wafanyikazi wapate mishahara bora," anasema.

"Nikifikiria jinsi babu yangu alivyohangaika kwa ajili yetu na jinsi alivyojitolea kwa ajili yetu, siwezi kuacha jitihada zake ziende bure na kwa kweli nataka kutetea wafanyikazi kama alivyofanya  kwa ajili ya kuhakikisha wafanyakazi ambao wanajaribu tu kupata riziki na kupata pesa wanakuwa na maisha bora na  familia zao zina maisha mema.”

Payman anataka kukabiliana na wapinzani wa Hijabu

Payman atajiunga na Seneti wakati huo huo seneta wa chama cha One Nation Moja Pauline Hanson akichaguliwa tena, ambaye aliwahi kuvaa burqa katika Seneti kama sehemu ya sarakasi ya kisiasa akitaka kupigwa marufuku kwa vazi la Kiislamu la Hijabu.

Payman anasema sasa akiwa katika seneti  labda atamfundisha kuhusu Hijabu ambayo anaivaa.

Ingawa Payman hajiishughulishi sana na historia  aliyoweka kama seneta kwa kwanza mwenye  kuvaa Hijabu Australia, anasema kwamba utambulisho wake daima utakuwa wa "Australia kwanza", akisema bado anashangazwa na jinsi alivyokubali nchi yake mpya baada ya kuwasili kama msichana  mwenye umri wa miaka minane.

"Ndiyo, mimi ndiye mwanamke wa kwanza aliyevaa Hijabu bungeni, lakini ni maadili ya chama change cha Leba ndiyo yaliyonifikisha hapa," anasema.

Anasema "ana imani" kwamba serikali mpya ya chama cha Leba itafanya zaidi kuboresha matibabu ya wahamiaji na wakimbizi nchini Australia na pia kwa wale walio kizuizini nje ya nchi. Pia anataka kutilia mkazo katika masuala ya gharama ya maisha, utunzaji wa watoto, mabadiliko ya hali ya hewa na masuala mengine yanayoathiri familia za vijana.

3479391

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :