Picha za tukio hilo, ambazo zilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii, zinaonyesha mwanamke huyo akikabiliana na mwingine kutokana na kauli mbiu ya "kutoka mtoni hadi baharini" iliyoonyeshwa kwenye fulana. Katika video hiyo, anasikika akihoji, "Je, unajivunia kuvaa 'kutoka mtoni hadi baharini'?"
Nara ya 'kutoka mtoni hadi baharini' hutumiwa na watetezi wa ukombozi wa Palestina wakiashiria kukombolea ardhi za Palestina zilizo baina ya Mto Jordan na Bahari ya Mediterenia.
Mwanamke Mwislamu aliyehusika, aliyetambulika kwa jina la Mariam na kuelezwa na wafuasi wake kama mtetezi wa haki za Wapalestina, alidaiwa katika mahojiano yaliyofuata yaliyotolewa na wanaharakati wanaoiunga mkono Palestina kwamba mwanamke huyo alitoa ishara za kutisha za mkono, ikiwa ni pamoja na kuiga mfano wa kukata koo huku akimrushia msannnnduku ya bidhaa.
"Alitishia kuniua. Binti yangu alikuwepo pia, jambo ambalo lilikuwa la kutisha," Mariam alisema wakati wa mahojiano. "Sikujua jinsi ya kumlinda, na alinifuata. Alikuja moja kwa moja usoni mwangu, moja kwa moja hapa."
Polisi walithibitisha kuwa maafisa walijibu ripoti za matusi na vitisho katika kituo cha biashara mwendo wa saa kumi jioni. siku ya Ijumaa.
Kufuatia uchunguzi, mwanamke mwenye umri wa miaka 39 alishtakiwa kwa kutishia ghasia hadharani kwa misingi ya kidini. Mamlaka ilisema mshtakiwa alinyimwa dhamana na aafiishwa katika Mahakama ya Mtaa ya Parramatta.
Tukio hili linatokea dhidi ya hali ya kuongezeka kwa matukio ya chuki dhidi ya Uislamu nchini Australia. Katika siku za hivi majuzi, matukio mengine mawili yameibua wasiwasi wa umma: maandishi ya kupinga Uislamu yaligunduliwa katika kitongoji cha Sydney cha Sefton, na lori lililokuwa na bendera za Palestina lilichomwa moto huko Melbourne magharibi mwa Melbourne.
3491164