IQNA

Kombe la Dunia Qatar

Msikiti Nchini Qatar wawavutia wasio Waislamu wakati wa Kombe la Dunia

15:01 - November 28, 2022
Habari ID: 3476165
TEHRAN (IQNA) – Msikiti Mkuu wa Katara (Msikiti wa Bluu) ni miongoni mwa vivutio vingi katika Kijiji cha Utamaduni cha Katara huko Doha, Qatar, ambacho sasa ni kivutio kikuu kwa watalii wakati wa Kombe la Dunia nchini humo.

Kwa ujumle Qatar imevutia watalii wengi kuwahi kushuhudiwa nchini humo kutokana na kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la FIFA 2022, haswa wageni wasio Waislamu ambao wameuvtiwa sana na ule mwito wa Sala misikitini unaojulikana kama Adhana. Wengi wamekuwa wakifika katika eneo la nje la  msikiti huo na kupiga picha za ukumbusho.

Kijiji cha Utamaduni cha Katara kimeshuhudia maelfu ya wageni kila siku wakiwa ili kujionea shughuli za sanaa, utamaduni na burudani sanjari na Kombe la Dunia la FIFA la Qatar 2022.

Wakuu wa eneo hilo wameweka chumba cha mapumziko karibu na msikiti ambacho pia kina bango linalosema: "Niulizeni kuhusu wanawake wa Qatar." Katika sebule, wanawake wa kigeni wanaweza kuketi na kunywa chai na kahawa, na kujifunza kuhusu maisha ya kijamii nchini Qatar. Mafunzo hayo yanatolewa na  watu waliojitolea kujibu maswali yao.

Mmoja wa waliojitolea ni Umm Ahmed na anasema: "Lengo la kuandaa mahali hapa karibu na msikiti ni kuwatambulisha wageni kuhusu utamaduni wa Qatar wa mavazi, vyakula na vinywaji, mila na desturi, na maswali yao mengi ni juu ya uhusiano wa kijamii wa familia ya Qatar na mila ya ndoa. .. Maswali yao ya kijamii zaidi yanahusu maisha ya Mwislamu kwa kuzingatia maadili ya Kiislamu. Wengi wa wageni wanakiri kwamba mtazamo wao juu ya Uislamu na Waislamu ulichafuliwa na chuki nyingi zisizo na msingi, lakini kuwa Qatar kumesaidia kubadilisha maoni yao digrii mia na themanini.

Katika lango la msikiti huo, kuna wafanyakazi na wahubiri kutoka Kituo cha Wageni cha Qatar ili kuutambulisha Uislamu. Wanapokea wasiokuwa Waislamu na kujibu maswali na maulizo yao kuhusu msikiti. Pia hupanga kuingia kwao msikitini baada ya sala za jamaa ili watu wapate kujua mazingira ya ndani ya msikiti.

Ikiwa nchi ndogo zaidi kuwahi kuandaa tukio kubwa zaidi la soka duniani, Qatar, ni nchi tajiri ya Ghuba ya Uajemi ambayo ni mzalishaji mkubwa wa gesi. Qatar imetumia vizuri fursa iliyojitokeza ya Kombe la Dunia kuarifisha dini tukufu ya Kiislamu kwa wageni waliofika nchini humo.

3481432

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha