IQNA

Sherehe zafanyika Mauritania kuwaenzi wahifadhi wa Qur'ani

21:59 - May 20, 2025
Habari ID: 3480713
IQNA – Kundi la watu waliokamilisha kuhifadhi Qur'anI Tukufu kikamilifu wameenziwa katika sherehe iliyofanyika katika mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott.

Sherehe hiyo iliandaliwa na Kituo cha Imam Warsh cha Kuhifadhi Qur'ani na Sayansi za Kidini siku ya Jumapili jioni.

Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Mauritania, Sidi Yahya Ould Cheikhna Ould Lemrabet, alihutubia hafla hiyo, akitambua juhudi za kituo hicho katika kuhimiza kuhifadhi Kitabu Kitakatifu.

Akibainisha kuwa wizara yake pia imechukua hatua katika mwelekeo huu, alisema kuwa juhudi hizi zinasaidia kuhifadhi utambulisho wa Kiislamu na kuwalinda vijana dhidi ya tabia hatarishi za kijamii.

Idara ya Masuala ya Kiislamu na Elimu ya wizara hiyo imehimiza kufunguliwa tena kwa vituo na shule nyingi, na idadi ya vituo hivyo imefikia 10,720 mwaka huu.

Sayed Mukhtar Ould Al-Khalifa, mwenyekiti wa baraza la usimamizi wa kituo hicho, pia alisema kuwa tangu kuanzishwa kwake, kituo hicho kimejitahidi kufundisha Quran kwa makundi yote ya jamii, hasa wasichana wenye kiwango cha chini cha elimu.

Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ni nchi iliyoko katika eneo la Maghreb la Afrika Kaskazini Magharibi.

Idadi ya watu wa nchi hiyo inakadiriwa kuwa takriban milioni 4, na karibu Wamauritania wote ni Waislamu.

Shughuli na programu za Quran ni maarufu sana katika nchi hiyo ya Afrika.

3493151

captcha