Wizara ya Masuala ya Kiislamu na Elimu Asilia ya nchi hiyo ilizindua rasmi mpango huo Jumapili katika mji mkuu wa Nouakchott. Mpango huo unalenga kuchangia katika kuitumikia na kuitukuza Kitabu cha Mwenyezi Mungu kupitia mradi unaonuia kuinua hadhi yake katika fikra za vizazi vinavyokuja.
Mradi huu unalenga kuwakinga vijana kwa mafundisho ya Qur'ani Tukufu na kuimarisha maadili yake tukufu yanayohimiza udugu na mshikamano, mbali na migogoro na kurudi nyuma kimaendeleo.
Wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Mwongozo wa Kiislamu, Mohamed Lamine Ould Cheikhna, alieleza kuthamini kwake kazi hii, ambayo ni sehemu ya kuitumikia Qur'ani Tukufu, na akamshukuru Rais wa Jamhuri Mohamed Ould Cheikh Ghazouani kwa maelekezo yake yanayoonesha hamasa ya serikali katika kuwatumikia Wamauritani na fani ya elimu ya Kiislamu kwa ujumla.
Mradi huo ulizinduliwa mbele ya maimamu na wasomaji kadhaa wa Qur'ani, pamoja na kundi la watu mashuhuri katika nyanja za kidini na kielimu.
Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ni nchi iliyoko katika ukanda wa Maghreb, Afrika ya Kaskazini-Magharibi. Idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kufikia milioni 4, na karibu Wamauritani wote ni Waislamu. Shughuli na programu za Qur'ani ni maarufu sana katika nchi hiyo ya Kiafrika.
3493066