Kwa mujibu wa tovuti ya al-Siraj, tukio hili la kitaifa la Qur’ani limeandaliwa na Idhaa ya Mauritania.
Msikiti Mkuu wa Nouakchott ni mwenyeji mashindano haya, ambayo yanajumuisha washiriki wa kiume na wa kike.
Jumla ya washiriki 1,950, wakiwemo mahafidh na wasomaji wa Qur’ani, wanashiriki katika mashindano haya kwa makundi mawili ya wanaume na wanawake.
Waziri wa Mambo ya Kiislamu, Sidi Yahya Ould Cheikhna Ould Lemrabet, pamoja na Waziri wa Utamaduni, Sanaa, Mawasiliano, na Mahusiano Al-Hussein Ould Medou, walihudhuria hafla ya ufunguzi.
Katika hotuba yake, Waziri wa Mambo ya Kiislamu alisisitiza umuhimu wa shindano hili katika kuhamasisha ushindani mzuri miongoni mwa vijana na kulitukuza mwezi wa Ramadhani kama mwezi wa Qur’ani.
Lemrabet aliwashukuru waandaaji wa mashindano haya na kusema:
“Nimefuatilia kwa karibu makundi ya mashindano na viwango vya washiriki. Uwazi ni sifa kuu ya shindano hili, inayodumishwa tangu usajili hadi kutangazwa kwa matokeo ya mwisho.”
Mkurugenzi wa Idhaaya Mauritania, Mohammad Abdul Qadir Ould, pia alizungumza katika hafla hiyo.
Alisema kuwa ongezeko la idadi ya washiriki ni moja ya sifa kubwa za shindano la mwaka huu, ambapo idadi imeongezeka kutoka 1,300 hadi 1,950.
Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ni nchi iliyoko katika eneo la Maghreb, kaskazini-magharibi mwa Afrika.
Idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa takriban milioni nne, na karibu Mauritania wote ni Waislamu.
Shughuli na programu za Qur’ani ni maarufu sana nchini humo.
3491900