IQNA

Qur'ani Barani Afrika

Washindi wa Mashindano ya Qur'ani Mauritania waenziwa

17:45 - December 01, 2024
Habari ID: 3479832
IQNA - Sherehe ilifanyika mapema wiki hii kuwatunuku washindi wa mashindano ya 11 ya kitaifa ya Qur'ani Mauritania.

Jumla ya wahifadhi na wasomaji Qur'ani 63 walitunukiwa kwa kushinda kategoria tofauti za mashindano hayo.

Pia waliotunukiwa katika hafla hiyo ni wajumbe wa kamati ya maandalizi na wataalamu na maqari walioshiriki katika warsha za elimu ya Ramadhani.

Hafla hiyo iliyoandaliwa na Redio ya Qur'ani ya Mauritania, ilihudhuriwa na Rais wa nchi hiyo ya Kiafrika Mohamed Ould Ghazouani na Waziri wa Utamaduni, Sanaa za Mikono na Mahusiano El Houssein Ould Medou.

Medou alisema katika hotuba yake kwamba shindano hilo halikuandaliwa kwa ajili ya kutoa tu zawadi bali ni fursa ya kuhuisha utiifu na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kutekeleza mafundisho na maadili ya Qur'ani katika maisha.

Katika hotuba yake, Medou pia alisifu nafasi ya Redio ya Qur'ani katika kukuza utamaduni wa Kiislamu na kuunga mkono utambulisho wa kitamaduni wa nchi.

Jumla ya wahifadhi na wasomaji Qur'ani 1,300 walishiriki katika mashindano ya 11 ya kitaifa ya Qur'ani Mauritania.

Idadi ya wataalamu wakuu wa Qur'ani kutoka sehemu mbalimbali za nchi walitathmini maonyesho yao na kuwachagua wagombea wakuu.

Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ni nchi iliyoko katika eneo la Maghreb magharibi mwa Afrika Kaskazini.

Idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa takriban milioni 4 na takriban Wamauritania wote ni Waislamu.

Shughuli na programu za Qur'ani ni maarufu sana katika nchi ya Kiafrika.

3490879

Habari zinazohusiana
captcha