IQNA

Waislamu Ufaransa

Msikiti wa Paris walalamika dhidi ya mwandishi wa Ufaransa aliyetoa kauli dhidi ya Uislamu

11:44 - December 30, 2022
Habari ID: 3476330
TEHRAN (IQNA) – Msikiti wa Jamia wa Paris, Ufaransa unawasilisha malalamiko ya jinai dhidi ya mwandishi Mfaransa Michel Houellebecq kutokana na kauli zake dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Uamuzi huo unaokuja huku kukiwa na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu nchini humo ulichukuliwa baada ya "mazungumzo marefu" kati ya Houellebecq na mwandishi mwingine, Michel Onfray. Mazungumzo hayo yalichapishwa katika jarida la Front Populaire mwezi Novemba, msikiti huo ulisema katika taarifa.

Katika makala hiyo, Houellebecq alisema kwamba watu nchini Ufaransa "wanajizatiti kwa silaha" na wanaweza kushambulia maeneo ya Waislamu.

"Watu wanajizatiti. Wananunua bunduki na kuchukua kozi za kufyatua risasi ... Nadhani mashambulizi yatatokea wakati maeneo yote yataanguka chini ya udhibiti wa Kiislamu. Kisha, mashambulizi na risasi zitafyatuliwa katika misikiti, migahawa inayotembelewa zaidi na Waislamu," alisema.

Kwa mujibu wa maafisa wa Msikiti wa Jamia wa Paris, "maneno yanayoumiza, hayakubaliki na ya kikatili sana."

"Hawatafuti kufafanua mjadala wowote wa umma lakini wanaibua matamshi na vitendo vya kibaguzi," iliongeza.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa ingawa kukosoa dini kunaruhusiwa katika jamii ya kidemokrasia, maoni katika kifungu hicho yalikuwa "yakitoa wito wa kuwapinga na kuwatenga Waislamu kwa ujumla."

"Katika mazingira haya, Msikiti wa Jamia wa Paris ulikuwa umeamua kuwasilisha malalamiko ... dhidi ya matamshi hayo ambayo inachukulia kama kitendo cha kuchochea chuki dhidi ya Waislamu," iliongeza.

Kufuatia kutekelezwa  sheria zinazowalenga Waislamu huko Ufaransa, hujuma dhidi ya Waislamu zimeongezeka sana.

Halikadhalika vituo vya Kiislamu vimekuwa vikishambuliwa mara kwa mara na watu wenye chuki ambao wamepata msukumo kutoka sera dhidi ya Uislamu za serikali.

Mwaka uliopita,  Bunge la Kitaifa la Ufaransa liliidhinisha sheria ya 'Thamani za Jamhuri' ambazo zilipendekezwa na rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo kwa ajili ya kukabiliana na kile alichokitaja ni 'Uislamu wa wanaotaka kujitenga.'

Jumuiya ya Waislamu Ufaransa (CFCM) imepinga vikali sheria hiyo na kuitaja kuwa yenye kuwawekea Waislamu vizingiti katika maisha yao yote.

Sheria hiyo inaipa serikali haki ya kuingilia mambo ya misikiti kama vile hotuba na kupeleleleza kamati zinazosimamia misikiti na pia kudhibiti matumizi ya pesa za misikiti na asasi za Waislamu.

3481869

Kishikizo: paris waislamu ufaransa
captcha