IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu Ufaransa

Muungano wa Misikiti Wamshitaki Mwandishi wa Riwaya Mfaransa Michel Houellebecq

22:19 - January 14, 2023
Habari ID: 3476404
TEHRAN (IQNA) – Mwandishi wa riwaya wa Ufaransa mwenye utata Michel Houellebecq anashtakiwa na Muungano wa Misikiti nchini Ufaransa kwa ubaguzi, matamshi ya chuki na kuchochea ghasia katika matamshi wakati wa mahojiano.

Houellebecq, ambaye vitabu vyake vinauzwa kwa wingi, aliandika riwaya ya mwaka 2015 iliyonyakua kichwa cha habari "Kujisalimisha" kuhusu uwezekano wa Muislamu kushinda urais, na hivyo kueneza hofu miongoni mwa wale wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia ambao huchochea chuki ya Uislamu.

Anashutumiwa kwa kumwambia mwandishi wa jarida la "Front Populaire" kwamba Waislamu nchini Ufaransa wanapaswa "kuacha kuiba na kuwa wakali" kwa  Wafaransa “asili”..

Aidha katika matamashi yake anasema  kwamba kunaweza kuwa na ghasia dhidi ya Waislamu wa Ufaransa, ghasia ambazo amezitaja kuwa "Bataclans reverse", ikiwa ni kumbukumbu ya mashambulizi ya mwaka 2015 kwenye jumba la tamasha la Bataclan ambayo yanadaiwa kutekelezwa wanamgambo wenye itikadi kali wa Ufaransa na wazaliwa wa Ubelgiji wanaohusishwa na kundi la kigaidi la Daesh.

Houellebecq amesema sehemu zenye utata zitahaririwa mtandaoni, na katika kitabu kijacho.

Mohammed Moussaoui, rais wa Muungano wa Misikiti nchini Ufaransa, alisema katika taarifa yake "pendekezo lake la kuzibadilisha katika kitabu kijacho halikomesha uenezaji wao na haliwakingi Waislamu kutokana na matokeo ya matamshi hayo".

Stephane Simon, mchangiaji wa "Front Populaire", ambaye alifanya mahojiano hayo na mwanafalsafa Michel Onfray, pia wametajwa kwenye kesi hiyo, wakili Najwa El Haite alisema.

captcha