IQNA

Jinai za Israel

Nchi 90 zaitaka Israel kukomesha hatua za adhabu dhidi ya Wapalestina uamuzi wa ICJ ukisubiriwa

16:57 - January 17, 2023
Habari ID: 3476415
TEHRAN (IQNA) - Zaidi ya nchi 90 zimeutaka utawala wa Kizayuni wa Israel kuacha hatua za kuwaadhibu Wapalestina kufuatia ombi la Umoja wa Mataifa la kutaka maoni ya ushauri kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ).

Mwishoni mwa mwezi Desemba, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kwa kupitisha azimio, lilitaka maoni ya ushauri ya Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) kuhusu namna utawala ghasibu wa Israel unavyokiuka haki ya Wapalestina ya kujitawala na kujiainishia hatima yao na utawala.

Katika upigaji kura, nchi 87 ziliunga mkono  azimio hili, nchi 26 zilipiga kura ya kupinga na nchi 53 hazikupiga kura.

Katika taarifa, watia saini walitaka kubadilishwa kwa hatua za Israeli, wakisema bila kujali msimamo wao juu ya azimio la Baraza Kuu, "tunapinga hatua za kuadhibu Wapalestina ambazo zimechukuliwa na Israel kama jibu kwa ombi la maoni ya ushauri wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki".

Katika kukabiliana na mpango uliofaulu wa Palestina katika Umoja wa Mataifa, serikali mpya ya Israel ya mrengo mkali wa kulia ilikamata dola milioni 39 ya mapato ya kodi yaliyokusanywa kwa niaba ya Mamlaka ya Palestina (PA).

Taarifa iliyotolewa na PA kwenye akaunti yake ya Twitter ilitiwa saini na wawakilishi wa mataifa ya Kiarabu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu yenye wanachama 57, pamoja na nchi nyingine 37, zikiwemo Ujerumani, Ufaransa, Italia, Japan, Korea Kusini, Brazil, Mexico na Africa Kusini.

Mapema mwezi huu, Israel pia ilimpiga marufuku waziri wa mambo ya nje wa Palestina, Riyad Maliki, kuondoka katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu ili kumzuia kukutana na viongozi wa kigeni.

Maoni ya ICJ yenye makao yake The Hague, ambayo yanasuluhisha mizozo kati ya nchi, ni ya lazima yatekelezwe, lakini mahakama haina uwezo wa kuwajibisha nchi kuyatekeleza. Maamuzi yake, hata hivyo, yana ushawishi mkubwa katika uga kimataifa.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ameliambia baraza lake la mawaziri kwamba hatua dhidi ya Wapalestina zinalenga kukabiliana kile alichokiita "hatua kali dhidi ya Israel" katika Umoja wa Mataifa.

Utawala haramu wa Israel siku ya Jumanne ulivamia miji kadhaa ya Palestina, ikiwa ni pamoja na Al Khalil au Hebron, Nablus, Ramallah, na Jenin na na kuharibu makazi sambamna na kuwakamata Wapalestina.

Katika kukabiliana na uvamizi huo, baadhi ya makundi yenye silaha ya Palestina yaliyafyatulia risasi wanajeshi wa Israel. Hata hivyo, hakuna Wapalestina au Waisraeli walioripotiwa kuuawa au kujeruhiwa.

Siku ya Jumatatu, jeshi la Israel lilimuua kijana wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 14 karibu na mji wa Beit Lahm au Bethlehem unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Israel.

Vikosi katili vya Israel viliwaua Wapalestina tisa wiki iliyopita. Hadi sasa mwaka huu, Wapalestina 14 wameuawa, wakiwemo watoto watatu.

Takriban 167 waliuawa mwaka jana katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, idadi kubwa zaidi ya vifo tangu Intifada ya Pili.

Vikosi vya utawala haramu wa Israel vinaendesha operesheni za karibu usiku za kusaka na kukamata katika Ukingo wa Magharibi, ambazo mara nyingi huwa mbaya.

Katika miezi ya hivi karibuni, uvamizi mwingi umelenga Nablus na Jenin katika miezi ya hivi karibuni, ambapo upinzani wa silaha wa Palestina unakua kwa zamu.

3482111

Habari zinazohusiana
captcha