IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Lita 40 za Maji ya Zamzam kusambazwa Mwezi wa Ramadhani Saudia

17:24 - March 17, 2023
Habari ID: 3476720
TEHRAN (IQNA) – Maafisa wa Saudi Arabia wanasema zaidi ya lita milioni 40 za maji ya Zamzam zitasambazwa katika Msikiti Mkuu wa Makka (Masjid al-Haram) miongoni mwa Mahujaji katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Takriban vituo 20,000 vimetengwa katika Msikiti Mkuu, eneo takatifu zaidi la Uislamu ambalo liko Saudi Arabia, ili kusambaza zaidi ya lita milioni 40 za maji matakatifu ya Zamzam kwa waumini wakati wa Ramadhani kuanzia wiki ijayo, afisa mmoja alisema.

Mwezi wa Ramadhani huwa kilele cha Umrah au hija ndogo katika Msikiti Mkuu huko Makka.

Mkuu wa idara ya Zamzam katika Msikiti Mkuu Abdul Rahman Al Zahrany alisema mitungi 30,000 ya Zamzam imetawanywa katika eneo hilo ili kuwapa waumini fursa ya kupata maji matakatifu kwa urahisi.

"Kurugenzi imeajiri wafanyakazi 1,423 ili kuhakikisha ufanisi na huduma bora," alinukuliwa na shirika la habari la Saudi SPA akisema.

Urais Mkuu wa Masjid al-Haram umetangaza umeweza kupiga hatua ya kiteknolojia"ubora wa kwa kutumia roboti pamoja na mikokoteni 80 mahiri katika usambazaji wa maji ya Zamzam katika msikiti mzima.

 "Wafanyikazi wetu wataimarisha usimamizi na ufuatiliaji, kuchukua sampuli za maji na kuzituma kwa maabara yetu ili kuhakikisha ubora wa maji," alisema Al Zahrany.

Roboti zilitumika wakati wa Hija ya mwaka jana kusambaza chupa za Zamzam kwenye Msikiti Mkuu kama sehemu ya tahadhari dhidi ya COVID-19.

Maji ya Zamzam ni maarufu kwa mahujaji wa kigeni ambao huyabeba kama zawadi kwa jamaa na marafiki baada ya kurudi nyumbani.

3482841

captcha