IQNA

22:58 - July 15, 2021
News ID: 3474103
TEHRAN (IQNA)- Idara ya Usimamizi wa Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina imeazimia kutumia maroboti katika Msikiti Mtakatifu wa Makka katika ibada ya Hija mwa huu.

Idara hiyo imesema roboti zitatumika kusafisha msikiti kwa kutumia kemikali maalumu za kuu virusi na halikadhalika kuwachunguza mahujaji ili kuhakikisha hawana alama za ugonjwa wa corona. Halikadhalika roboti hizo zinatazamiwa kutumika katika kusambaza maji ya Zamzam.

Wizara ya Hija na Umra ya Saudi Arabia imetangaza kuwa, ibada ya Hija mwaka huu itafanyika kwa kushirikisha raia na wageni wanaoishi nchini humo na kwamba watakaoruhusiwa Kuhiji hawatazidi  elfu 60.

Mwaka jana pia Waislamu wasiozidi elfu 10 wanaoishi ndani ya Saudia kwenyewe ndio walioruhusiwa kushiriki katika ibada ya Hija ambayo kwa kawaida huhudhuriwa na Waislamu zaidi ya milioni mbili kila mwaka kutoka maeneo mbalimbali ya dunia.

Jumuiya ya Maulama wa Yemen imelaani uamuzi uliochukuliwa na Saudi Arabia wa kuzuia ibada ya Hijja na Umra kwa Waislamu kutoka nje ya nchi hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo.

Taarifa iliyotolewa na jumuiya hiyo imesema kuwa, uamuzi wa serikali ya Riyadh wa kuzuia ibada ya Hija kwa mwaka wa pili mfululizo kwa kutumia kisingizio cha maambukizi ya virusi vya corona umechukuliwa kwa shabaha ya kuihudumia Marekani na Israel. 

Taarifa ya Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini Yemen imesema uamuzi huo wa kuzuia ibada ya Hija mwaka huu unaenda sambamba na malengo ya Marekini na Israel na si ajabu kwamba umebuniwa na kupikwa Washington na Tel Aviv.

3475254

Tags: saudia ، makka ، hija
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: