IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Rais Ruto wa Kenya atuma salamu za aina yake za Ramadhani kwa Waislamu + Video

6:56 - March 24, 2023
Habari ID: 3476754
TEHRAN (IQNA)- Rais William Ruto wa Kenya amewatumia Waislamu salamu za kheri na fanaka kwa mnasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka 1444 Hijria Qamaria.

Salamu za rais wa Kenya mwaka huu zilikuwa  za aina yake kwani zimekuja katika muundo wa mazungumzo na watoto wawili Waislamu katika Ikulu ya Rais mjini Nairobi. Rais Ruto amezungumza na watoto hao kuhusu Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na umuhimu wa Saumu katika mwezi huu. Rais Ruto amesema yeye kama Mkristo anafahamu Saumu ya Ramadhani na kuongeza kuwa kuna nukta nyingi za pamoja katika Qur'ani Tukufu na Bibilia.

Baada ya mazungumzo hayo yenye mvuto wa aina yake, Rais Ruto alichukua fursa hiyo kuwatumia Waislamu salamu za kheri na fanaka kwa mnasaba wa kuwadia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Hii hapa klipu hiyo ya Rais wa Kenya

captcha