TEHRAN (IQNA)- Wapigania ukombozi wa Palestina leo wametekeleza operesheni kubwa zaidi na ya kihistoria dhidi ya utawala dhalimu na wa kikoloni wa Israel ambapo idadi kubwa ya wanajeshi wa Kizazyuni na walowezi wa Kizayuni wameangamizwa.

Tawi la kijeshi la Hamas limesema zaidi ya makombora 7,000 yamerushwa kutoka Ukanda wa Gaza mapema leo kuelekea ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, na kutangaza kuwa limeanzisha "Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa".
"Tumeamua kukomesha uhalifu na jinai zote za maghasibu. Wakati wao wa kufanya fujo na kujifaragua bila ya kuwajibishwa umekwisha," imesisitiza taarifa hiyo ya Izzuddin al Qassam.
Wakati huouo Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina imetangaza kuwa wapiganaji wake wamejiunga na operesheni hiyo ya Kimbunga cha Al-Aqsa huku Hamas ikitoa wito kwa Wapalestina kila mahali walipo kujiunga na mapambano na kuyataka makundi ya Muqawama nchini Lebanon pia kujiunga na vita dhidi ya Israel.
"Sisi ni sehemu ya vita hivi, wapiganaji wetu wako bega kwa bega na ndugu zao katika Brigedi za Qassam hadi ushindi upatikane," ameeleza Abu Hamza, msemaji wa tawi la kijeshi la Jihadul-Islami kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram.