IQNA

Jinai za Israel

Utawala katili wa Israel umetekeleza mauaji makubwa dhidi ya Wapalestina katika kambi ya Jenin

15:36 - July 05, 2023
Habari ID: 3477241
AL-QUDS (IQNA) - Jeshi la utawala wa Kizayuni usiku wa kuamkia Jumatatu lilianzisha mashambulio makubwa dhidi ya mji na kambi ya wakimbizi ya Jenin ya Wapalestina. Magari 150 ya kijeshi na askari 1000 wa majeshi ya polisi, magenge ya kijasusi ya Kizayuni na polisi wa mpakani wa Israel wameshiriki kwenye uvamizi huo.

Jana Jumanne utawala wa Kizayuni ulianza kutumia ndege za kivita kushambulia mji na kambi ya wakimbizi ya Jenin huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Makumi ya Wapalestina walikuwa wameuawa na kujeruhiwa na maelfu ya wengine walikuwa tayari wamelazimika kukimbia makazi yao hadi wakati tulipokuwa tunaandaa uchambuzi huu wa kisiasa.

Wanaharakati wa vyombo vya habari wameripoti hali mbaya na ya kutisha katika maeneo ya Jenin. Picha na video za wanaharakati hao zinaonesha jinsi majasusi wa Israel walivyokuwa wanatumia mabomu ya kila namna kuzishambulia familia za Wapalestina na kuwalazimisha kutoka majumbani mwao hata wananchi wa kawaida ambao walikuwa wametumia nyumba zao kujikinga na jinai hizo mpya za Wazayuni.

Kabla ya hapo, ripoti zilibaini kwamba kambi ya wakimbizi ya Jenin inashuhudia familia za Wapalestina zikitoka kwa lazima na kwa mkumpuo, kiasi kwamba wakati anaripoti habari hiyo, zaidi ya familia 500 zilikuwa zimeondoka eneo hilo. 

Meya wa mji wa Jenin, Muhammad Jarrar amesema kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni lizazipiga kwa mabomu na kwa makusudi nyumba za Wapalestina ili kuziharibu licha ya kuwemo humo wanawake, watoto wadogo na watu wa kawaida na limewalazimisha wakazi wengi wa mji wa Jenin kukimbia nyumba zao. 

Maafisa wa manispaa ya Jenin wamesisitiza kuwa, jeshi la Israel limefanya uharibifu mkubwa katika nyumba za kambi ya wakimbizi ya Jenin kiasi kwamba utadhani kumetokea tetemeko kubwa la ardhi katika maeneo hayo.

Wamesema, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wameshindwa kukabiliana na wanamuqawama wa Palestina hivyo wanamalizia hamaki zao kwenye kuua watu wasio na hatia, kuharibu miundombinu na kuvunja nyumba za raia wa kawaida. Wamesisitiza kuwa, wanajeshi wa Israel wana orodha ya maeneo walipo wanamuqawama wa Palestina lakini kwa vile wanaogopa kupambana nao moja kwa moja, wanaamua kuharibu miundombinu ya umeme na ya maji ili kuwaweka kwenye wakati mgumu wananchi wa kawaida.

Si hayo tu lakini pia utawala wa Kizayuni unazuia kufikiwa na misaada ya dharura Wapalestina 19,000 wa eneo hilo la Jenin ambalo lina wagonjwa wengi vizee na wasiojiweza.

Madaktari wasio na mipaka huko Jenin wanasema kuwa, viongozi wa Israel ni waongo wanaposema kuwa wanajeshi wao wanashambulia tu miundomboni ya kijeshi katika kambi ya wakimbizi ya Jenin.

Mkuu wa shirika la Hilal Nyekundu la Palestina amesema, hali ya kibinadamu katika kambi ya wakimbizi ya Jenin ni mbaya sana. Wakazi wa eneo hilo hivi sasa wanahitajia mno maji na chakula lakini wanazuiwa na wanajeshi wa Israel.

Baadhi ya waandishi wa habari ambao hivi sasa wako Jenin wameripoti kuwa, wanajeshi wa Israel wametumia risasi za kivita kuwashambulia waandishi hao. Hii si mara kwanza kwa wanajeshi makatili wa Israel kukanyaga sheria zote zinazowalinda waandishi wa habari. Mwaka jana, mwandishi wa habari wa televisheni ya Al Jazeera, Shireen Abu Akleh mbaye alikuwa ni Mpalestina-Mmarekani alipigwa risasi kwa makusudi na kuuliwa kidhulma na wanajeshi wasio na huruma wa Israel. Tangu mwaka 2000 hadi hivi sasa, wanajeshi Wazayuni wameshaua waandishi wa habari wasiopungua 45 huko Palestina.

Mashambulio ya hivi sasa ya utawala wa Kizayuni huko Jenin yanahesabiwa kuwa ni mashambulizi makubwa zaidi ya jeshi la Israel dhidi ya kambi hiyo ya wakimbizi wa Palestina tangu mwaka 2002 wakati ilipoanza Intifadha ya Pili ya Wapalestina. Mwezi Aprili 2002 Israel iliendesha operesheni iliyoipa jina la "Ngao ya Ulinzi" na kufanya jinai kubwa dhidi ya kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Jenin. Katika opereseheni hiyo, Wazayuni makatili waliharibu nyumba 535 za Wapalestina, 455 kati yake waliziharibu kikamilifu na waliua shahidi Wapalestina 58 wengi wao wakiwa si sehemu kabisa ya wapiganaji wa Palestina. Wanamapambano wa Palestina walifanikiwa kuangamiza wanajeshi 50 Wazayuni katika operesheni hiyo na kujeruhi makumi ya Wazayuni wengine.

3484211

Habari zinazohusiana
Kishikizo: jinai za israel
captcha