IQNA

Jinai za Israel

Wapalestina wataka hatua zichukuliwe dhidi Waziri wa Fedha wa utawala wa Kizayuni wa Israel

18:30 - March 21, 2023
Habari ID: 3476739
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeiomba Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutoa hati ya kukamatwa Waziri wa Fedha wa utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na matamshi yake dhidi ya Palestina.

Bezalel Smotrich, Waziri wa Fedha wa utawala wa Kizayuni amedai katika kikao cha Paris kwamba "hakuna kitu kinachojulikana kama watu wa Palestina". Amedai kuwa, watu wa Palestina ni jambo lililoanzishwa katika karne iliyopita na kwamba watu kama yeye na mababu zake ndio Wapalestina halisi.

Hapo awali Waziri huyo wa Fedha wa utawala wa Kizayuni wa Israel aliunga mkono mashambulizi yanayofanywa na walowezi wa Kiyahudi dhidi ya Wapalestina katika eneo la Hawara kusini mwa Nablus na kutoa wito wa kufutwa kabisa Wapalestina wakazi wa eneo hilo.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Palestina pia imeeleza masikitiko yake kwa hatua ya maafisa wa serikali ya Ufaransa kumruhusu Smotrich kutoa matamshi ya kibaguzi na kifashisti kwenye ardhi ya Ufaransa.

Wakati huo huo Wizara ya Mambo ya Nje ya Jordan pia imemwita na kumsaili balozi wa utawala haramu wa Israel kutokana na matamshi ya Waziri wa Fedha wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina.

Mapema mwezi huu wa Machi Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, alilaani matamshi ya kibaguzi na kiichochoze yaliyotolewa na Waziri wa Fedha wa Israel akitaka kufutwa kabisa kitongoji cha Huwara cha Wapalestina katika uso wa dunia.

Smotrich alisema: "Kijiji cha Hawara lazima kifutiliwe mbali. "Naamini kwamba jambo hili linapaswa kufanywa na serikali ya Israeli na sio watu wa kawaida."

3482884

captcha