IQNA

Jinai za Israel

Jenerali Mzayuni: Jeshi la Israel yumkini likaangamia katika vita vijavyo

19:43 - September 01, 2023
Habari ID: 3477533
TEHRAN (IQNA)-- Meja Jenerali mstaafu wa Israel ameonya juu ya uwezekano wa kuangamia jeshi la utawala huo haramu iwapo litajitosa katika vita vipya.

Meja Jenerali (Mstaafu), Israel Ziv ambaye alikuwa Kamanda wa Kikosi cha Operesheni cha jeshi la Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ametoa indhari hiyo kama radimali yake kwa hali ya taharuki iliyotanda katika kijiji cha Ghajar kilichoko katika mpaka wa Israel na Lebanon.

Kamanda huyo mwandamizi wa zamani wa Israel amemtaka Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjain Netanyahu kuchukua hatua za kuzuia makabiliano yoyote mapya ya kijeshi.

Amesema taharuki katika uzio wa mpaka baina ya Lebanon na maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel imeulazimisha utawala wa Tel Aviv kufuatilia sera ya kujizuia, ili kujiepusha na kile alichokitaja kuwa uchokozi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

Ziv amedai kuwa, "Hizbullah na Iran zinatathmini na kufuatilia hali ndani ya Israel, na zinahisi kuwa Waisraeli wanapitia kipindi cha udhaifu hivi sasa."

Kabla ya hapo, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrallah aliwaonya viongozi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kwamba, mauaji yoyote yatakayofanywa ndani ya ardhi ya Lebanon dhiai ya raia wa Lebanon, Palestina au Iran au raia wa nchi nyingineyo hayatapita bila ya jibu.

Nasrullah hivi karibuni alionya pia kwa kusema, utawala huo wa Kizayuni utarejeshwa nyuma mamilioni ya miaka hadi enzi za mawe, iwapo utaingia katika vita vipya na Lebanon.

3484992

Habari zinazohusiana
Kishikizo: jinai za israel
captcha