IQNA

Jinai za Israel

Utawala wa Israel umebomoa majengo 56 ya Wapalestina katika kipindi cha wiki mbili

12:57 - August 17, 2023
Habari ID: 3477451
AL-QUDS (IQNA) - Takriban majengo 56 yanayomilikiwa na Wapalestina, zikiwemo nyumba sita, katika jiji la al-Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu na eneo C la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan zimebomolewa au kutekwa na utawala ghasibu wa Israel katika muda wa wiki mbili.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ilisema wiki hii kwamba ubomoaji na ukamataji ulifanyika kati ya Julai 25 na Agosti 7 kwa kisingizio cha kukosa vibali vya ujenzi ambavyo ni vigumu kupatikana.

Katika ripoti yake, bodi hiyo ilisema ubomoaji huo umesababisha Wapalestina kupoteza makazi yao, wengi wao wakiwa watoto, na kuathiri pato na mitaji ya kimaisha ya wengine 3,500.

Ripoti hiyo imesema majengo sita kati yaliyobomolewa yalikuwa yamejengwa kwa misaada ya wafadhili  katika kukabiliana na ubomoaji wa awali katika jamii ya Wabedouin ya Az Za'ayyem katika mkoa wa Al Quds.

Zaidi ya walowezi wa Kizayuni  700,000 wanaishi katika takriban vitongoji haramu 280 katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu tangu utawala wa Israel ulipokalia eneo hilo mwaka 1967.

Jumuiya ya kimataifa inayachukulia makazi hayo kuwa haramu chini ya sheria ya kimataifa na Mikataba ya Geneva ikizingatiwa kwamba yamejengwa katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu.

Vikosi vya Israel vimewaua Wapalestina 167 katika Ukingo wa Magharibi hadi sasa mwaka huu ambayo inazidi idadi ya jumla iliyorekodiwa mwaka jana.

Hii inafanya 2023 kuwa mwaka mbaya zaidi kwa Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi tangu 2005.

Umoja wa Mataifa unasema walowezi wa Israel pia wamewaua Wapalestina saba mwaka huu.

Habari zinazohusiana
Kishikizo: jinai za israel
captcha