IQNA

Wafanyaziara Milioni 5 watembelea Karbala wakati wa Idi ya Shaaban

17:23 - February 15, 2025
Habari ID: 3480223
IQNA – Zaidi ya wafanyaziara milioni tano kutoka Iraq na nchi nyingine walitembelea mji mtakatifu wa Karbala kwa ajili ya Idi ya Shaaban Ijumaa, afisa mmoja alisema.

Gavana wa Karbala Nasif al-Khatabi alisema katika mkutano wa pamoja na makamanda wa polisi na Operesheni ya Usalama ya Karbala, aliongeza kuwa idadi ya magari yaliyofika mkoa huo wakati wa kipindi cha sherehe hizo ambazo pia ni maarufu kama Nisf Shaaban, kama ilivyosajiliwa kupitia mfumo wa usafiri wa trafiki, ilizidi 533,000.

Alisema mipango ya usalama na huduma kwa ajili ya hafla hiyo ilitekelezwa kwa mafanikio. Al-Khatabi alibainisha kuwa mpango wa huduma ulitekelezwa katika nyanja za afya, usafiri na huduma zilizotolewa kwa wahujaji.

Idara ya Afya ya Mkoa wa Karbala hapo awali ilitangaza kupelekwa kwa timu za afya na maandalizi ya hospitali kwa ajili ya sherehe za hija ya Shaaban.

Idi ya Shaaban, inayoashiria kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Mahdi  (Mwenyezi Mungu aiharakishe faraja yake), inaangukia siku ya 15 ya mwezi wa Hijri wa Shaaban (Ijumaa, Februari 14, mwaka huu).

Waislamu wa madhehebu ya Shia kote ulimwenguni husherehekea hafla hiyo adhimu. Idadi kubwa ya wafanyaziara hutembelea kaburi la Imam Hussein (AS) siku kadhaa kuelekea tarehe 15 ya Shaaban.

3491863

Kishikizo: imam mahdi karbala
captcha