IQNA

Jinai za Israel

Maneno hayawezi kueleza ukatili wa Israel huko Gaza, asema afisa wa Umoja wa Mataifa

11:31 - March 01, 2024
Habari ID: 3478435
IQNA - Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kusikitishwa kwake na ukatili ambao utawala wa Israel imekuwa ukitekelezwa kwa miezi kadhaa vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Volker Turk aliliambia Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa huko Geneva siku ya Alhamisi kwamba inaonekana hakuna hakuna maneno yanayoweza kueleza maovu ambayo yanatokea mbele ya macho yetu huko Gaza.

Zaidi ya Wapalestina 30,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto wameuawa kutokana na mashambulizi ya jeshi dhalimu la Israel huko Gaza tokea Oktiba 7 hadi sasa.

Utawala haramu wa Israel ulianzisha vita hivyo mwaka jana kufuatia operesheni ya ulipizaji kisasi ijulikanao kama Kimbunga cha Al-Aqsa, dhidi ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Turk amelaani "ukatili wa majibu ya Israeli" kwa operesheni hiyo na kusema vita ambacyo Israel ilianzisha ni vya "kutisha na makosa kabisa."

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa, wakati huo huo, alionya juu ya matokeo mabaya iwapo utawala wa Kizayuni utaanzisha mashambulizi ya nchi kavu dhidi ya mji wa kusini wa Gaza wa Rafah.

Zaidi ya Wapalestina milioni 1.5 ambao ni sehemu ya wakazi milioni 2.4 wa Gaza wamekimbilia Rafah wakati wa vita kwa sababu hakuna mahali popote salama katika ukanda huo wa pwani.

Shambulio kama hilo la ardhini, Turk alisema, litakiuka maagizo yaliyotolewa na mahakama kuu ya Umoja wa Mataifa.

Mnamo Januari 26, Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) huko The Hague ilisema Israel inapaswa "kuzuia utekelezwaji wa vitendo vyote ndani ya wigo" wa Mkataba wa Mauaji ya Kimbari.

Wakati huo huo, Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa Riyad Mansour ametoa wito kwa Baraza la Usalama kulaani vifo vya zaidi ya Wapalestina 100 na kujeruhiwa kwa karibu watu 700 katika shambulio la kikatili la Israel dhidi ya umati wa watu waliokuwa wakisubiri chakula katika mji wa Gaza.

Riyad Mansour alitoa kauli hiyo mbele ya waandishi habari siku ya Alhamisi kabla ya mkutano wa faragha wa baraza hilo, ambao ulikuja kwa ombi la Algeria.

Mkutano huo ulifanyika kujadili hatua ya Israel kuwalenga raia wanaosubiri msaada wa kibinadamu huko Gaza. Wizara ya afya katika eneo hilo la pwani lililozingirwa ilisema watu 112 waliuawa katika shambulio hilo na wengine 760 kujeruhiwa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani wanajeshi wa Israel kwa kuwafyatulia risasi Wapalestina waliokuwa na njaa wanaosubiri msaada wa kibinadamu kusini mwa mji wa Gaza.

Watu walioshuhudia wameeleza kuwa mamia ya Wapalestina walikuwa wakisubiri kugawiwa misaada ya kibinadamu karibu na eneo lq Dowar al Nablusi wakati walipofyatuliwa risasi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni.

3487380

Habari zinazohusiana
captcha