Chuo Kikuu Huria cha Brussels, Ubelgiji kimetangaza kujiondoa katika mradi wa kisayansi wa Akili Mnemba (AI) ambao ulihusisha taasisi mbili za Israeli, Kituo cha Habari cha Palestina kiliripoti.
Chuo hicho kinaonekana kimechukua uamuzi huo kwa kuzingatia vita vya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatano, chuo kikuu hicho kilieleza kuwa uamuzi wa kujiondoa katika mradi huo wa kisayansi ulifanywa baada ya tathmini iliyofanywa na Kamati ya Maadili.
Iliendelea kusema kuwa, kufuatia matukio ya hivi karibuni huko Gaza, imeamuliwa kufanya mapitio ya kina ya miradi yote ya utafiti inayohusisha washirika wa Israel.
Chuo kikuu hicho kimekata uhusiano na Israel na sasa kimeazimia kuendeleza ushirikiano wake na taasisi za Palestina.
Wanafunzi kutoka chuo kikuu hicho wameshiriki katika maandamano ya kuunga mkono Palestina yaliyoanza Marekani na kuenea hadi Ulaya, kulaani mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na jeshi katili la Israel huko Gaza.
3488272