IQNA

Watetezi wa Palestina

Nchi zaendelea kuunga mkono Afrika Kusini katika kesi yake ICJ dhidi ya Israel kuhusu mauaji ya kimbari ya Gaza

10:36 - January 11, 2024
Habari ID: 3478182
IQNA- Nchi zaidi zimeungana na Afrika Kusini katika kesi iliyowasilishwa dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu vita vya mauaji ya kimbari vya utawala huo kwenye dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuunga mkono uamuzi wa Afrika Kusini wa kuwasilisha kesi dhidi ya utawala haramu wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu jinai za mauaji ya kimbari zinazotekelezwa na utawala huo dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, katika taarifa yake iliyotolewa siku ya Jumatano, imesema Israel, ikiwa na uungwaji mkono usio na masharti kutoka kwa baadhi ya serikali, imekuwa ikifanya mashambulizi makali ya kijeshi dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu katika kipindi cha miezi mitatu, na hivyo kukiuja mikataba yote ya kimataifa inayowahusu Wapalestina wanaodhulumiwa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine tena inalaani vikali jinai za kivita za utawala wa kibaguzi wa Kizayuni na mauaji ya kimbari dhidi ya taifa la Palestina, na kueleza uungaji mkono wake kwa mapmabano (muqawama) kama hatua ya ukombozi na haki halali inayotambuliwa na sheria za kimataifa kwa taifa la Palestina katika mapambano dhidi ya ukaliwaji mabavu ardhi zao."

Maldives, Namibia na Pakistan PIA zimetangaza kuunga mkono kesi ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Tel Aviv wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne.

Katika chapisho la mtandao wa kijamii, Ujumbe wa Kudumu wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa Islamabad imekaribisha mpango wa Afrika Kusini wa kuishtaki Israel chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mauaji ya Kimbari.

Neville Gertze, mwakilishi wa kudumu wa Namibia katika Umoja wa Mataifa, pia alisema nchi yake "inakaribisha na kuunga mkono" hatua za kisheria za Afrika Kusini.

Katika taarifa, serikali ya Maldives pia ilikaribisha ombi la Afrika Kusini mbele ya ICJ, huku ikisisitiza kwamba Israel inakiuka "Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari" wa 1948.

Afrika Kusini ilifungua kesi dhidi ya Israel mwishoni mwa mwezi Disemba, baada ya takriban miezi mitatu ya vita vya maangamizi ya umati vya Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Kesi hiyo ilisema hatua za Israel ni "mauaji ya kimbari kwa sababu zina nia ya kuleta uharibifu wa sehemu kubwa ya kundi la taifa, rangi na kaumu ya Palestina."

Ombi hilo pia lilisema mashambulizi ya Israel yanakiuka Mkataba wa Mauaji ya Kimbari ya Umoja wa Mataifa, na kuitaka mahakama hiyo "iamuru Israel isitishe mauaji na madhara makubwa ya kiakili na kimwili kwa Wapalestina huko Gaza."

Nchi nyingine ambazo tayari zimeonyesha kuunga mkono kesi hiyo ni pamoja na Bolivia, Jordan, Malaysia, Saudi Arabia na Uturuki. ICJ itaanza kusikiliza kesi hiyo Alhamisi na Ijumaa wiki hii.

3486765

 

Habari zinazohusiana
captcha