IQNA

Watetezi wa Palestina

Raisi uamuzi wa Afrika Kusini wa kuushtaki utawala wa Kizayuni katika mahakama ya ICJ

13:14 - January 27, 2024
Habari ID: 3478260
IQNA-Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mashtaka ya Afrika Kusini dhidi ya mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza yanapongezwa na kusifiwa na watu wote wanaopigania uhuru na ukombozi.

Rais wa Iran amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na kueleza kwamba nia ya maafisa wa nchi hizo mbili ni kuboresha zaidi uhusiano katika nyanja mbalimbali.

Sambamba na kupongeza hatua hatua ya kijasiri ya serikali ya Afrika Kusini katika kuwasilisha shauri la mashtaka dhidi ya utawala wa Kizayuni katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki amesema: Hatua hii inatoka kwa nchi ambayo imekumbwa na machungu ya ubaguzi wa rangi na mauaji ya kimbari kwa miaka mingi.

Aidha amesema, hatua hiii ya Afrika Kusini haisifiwi na kupongezwa tu katika ulimwengu wa Kiislamu bali katika mataifa yote ya ulimwengu ambayo yanapenda uhuru na haki.

Raisi ametangaza uungaji mkono madhubuti wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa hatua hiyo ya kijasiri ya Afrika Kusini na kuongeza: "Hatua hii itatambulisha jina lako Bw. Ramaphosa sambamba na jina la Nelson Mandela kuwa shakhsia inayopinga ubaguzi wa rangi na kusaka haki duniani wakati huu wa kutochukua hatua asasi za kimataifa.

Wakati huo huo, Ijumaa yaleo  tarehe 26 mwezi huu wa Januari mwaka 2024 huko The Hague, Uholanzi, Mahakama ya Kimataifa ya Haki inatoa uamuzi juu ya shauri la Afrika Kusini la kuitaka itoe agizo juu ya ombi lake la kutaka ichukue hatua za awali dhidi ya utawala wa Kizayuni Israel kutokana na mauaji yake ya kimbari huko Gaza dhidi ya Wapalestina.

4195987

Habari zinazohusiana
captcha