IQNA

Kombe la Dunia la Qatar

Usomaji Qur'ani Tukufu wa Mchezaji wa Timu ya Soka ya Morocco aliye katika Kombe la Dunia

22:14 - December 09, 2022
Habari ID: 3476224
TEHRAN (IQNA)-Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Soko ya Morocco, Abdel Razzaq Hamdallah hivi karibuni ameonekana akisoma Qur'ani Tukufu.

Klipu ya qiraa hiyo ya Qur'ani Tukufu imesambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii. 

Hamdallah na wenzake waliweka historia baada ya kupata ushindi mkubwa kwa kuwaondoa Uhispania kwa mikwaju ya penalti baada ya kutaka sare ya kutofungana katika Kombe la Dunia la FIFA 2022 nchini Qatar.

Wachezaji wa timu ya Morocco walisherehekea ushindi huo kwa kupeperusha bendera ya taifa linalokandamizwa na Israel la Palestina wakitangaza uungaji mkono wao kwa mapambano ya ukombozi wa Palestina na kibla cha kwanza cha Waislamu. Vilevile walionekana wakisuduju uwanjani wakimshukuru Mwenyezi Mungu kwa mafanikio hayo.  

Morocco ni nchi ya nne barani Afrika kufika hatua hii ya mashindano hayo, baada ya Cameroon, Senegal na Ghana. Timu ya Soka ya Morocco inayojulikana kama Simba wa Atlas itachuana na Ureno kesho Disemba 10 kuwania nafasi ya semi fainali.

4105458

captcha