Hamid Majidimehr, Mkuu wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Jumuiya ya Wakfu na Misaada aliiambia IQNA kwamba Saudi Arabia imetuma barua rasmi ya kuialika Iran kuwatambulisha wawakilishi wake katika mashindano hayo.
Itakuwa kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu ambapo Iran itashiriki katika tukio la Qur'ani la Saudia, alibainisha.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Saudi Arabia, pamoja na yale ya Iran na Malaysia, ni miongoni mwa mashindano kongwe na bora zaidi ya Qur'ani duniani, alisema.
Mashindano ya 44 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Saudi Arabia yanapangwa kufanyika katika siku za mwanzo za mwezi wa Agosti , na kuongeza kuwa Iran imeombwa kutambulisha wawakilishi wawili kwa tukio hilo la Qur'ani.
Kwingineko katika matamshi yake, Majidimehr amebainisha kuwa, maqari na wahifadhi Qur’ani wa Iran wameshinda nafasi takriban 400 katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani na kusisitiza kuwa, kuwepo kwa mafanikio wawakilishi wa Iran katika matukio ya kimataifa ya Qur'ani kunaashiria kukua kwa shughuli za Qur'ani nchini.
Iran na Saudi Arabia zilianzisha tena uhusiano wa kidiplomasia mnamo Machi 2023 baada ya kuvunja uhusiano mnamo 2016.
Baadaye, Aprili 2023, Yunes Shahmoradi kutoka Iran alinyakua tuzo ya juu katika toleo la pili la mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Otr Elkalam nchini Saudi Arabia.
4215997