Franc Romaneus amekuwa akijishughulisha na shughuli za kibinadamu katika kambi ya wakimbizi kwa miaka mingi.
Alikuwa mwanachama wa "Msafara wa Uhuru wa Meli “ ambao ulilenga kuvunja mzingiro kwenye Ukanda wa Gaza na kupeleka misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina katika eneo la pwani.
Franc anasema alijifunza Uislamu kwa mara ya kwanza alipokuwa Casablanca ya Morocco, Al Jazeera iliripoti.
“Sikuwa na dini wakati huo. Nilifadhaika sana na kuchanganyikiwa. Kisha nilirudi Ufaransa na baada ya miaka michache nikaenda Palestina,” alisema.
Kisha Wapalestina wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Jenin walimwalika ajiunge nao. "Walisema watanisaidia kuona nuru na kumpata Mwenyezi Mungu."
Kisha akaanza kusoma Qur’ani Tukufu kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri zake katika Kifaransa na Kiingereza na aliporejea Ufaransa, tayari alikuwa amesilimu.
Franc alisema sababu moja iliyomfanya apendezwe na Uislamu ni Imani thabiti ya wa Wapalestina pamoja na kuwa wanakumbana na masaibu kila siku.
Imani yao kwa Mwenyezi Mungu ni nguvu muhimu sana na hilo ndilo aliloamua kulifahamu zaidi hadi aliposilimu, alisema.
3488377