IQNA

Siku za Tashriq na Hija

9:45 - June 18, 2024
Habari ID: 3478974
Siku za Tashriq ni siku ya 11, 12 na 13 ya mwezi wa Hijri wa Dhul Hija ambapo ibada kuu za Hija kama dhabihu ya wanyama na Rami Al-Jamaratu hufanyika.

Kuna maoni tofauti kuhusu kuita siku hizi Tashriq, Wengine wanaamini kwamba ni kwa sababu baada ya dhabihu ya mnyama, nyama ingewekwa kwenye jua ili ikauke, na walihitaji mwanga wa jua na joto la kutosha kufanya hivyo.

Na pia Wengine wanasema; siku hizi zinaitwa Tashriq kwa sababu walianza kafara ya wanyama jua lilipochomoza. 
Suala muhimu lililo wazi ni kwamba jina la Tashriq lilianzia zama za Jahilliyah kabla ya kuja kwa Uislamu, Katika miaka ya mwanzo baada ya ujio wa Uislamu, kila moja ya siku hizi tatu ilikuwa na jina lake maalum.

Sadaka ya mnyama ni kitendo cha Wajib  yani lazima katika mila za Hija huko Mina, Mahujaji huitekeleza baada ya kuingia Mina katika Siku za Tashriq.

Miongoni mwa mila zingine za Wajibu ni wakati wa Siku za Tashriq ni Rami Al-Jamarat kupigwa mawe kwa shetani na kukaa Mina hadi usiku wa manane.

Rami Al-Jamarat inaonyesha Mapambano dhidi ya Shetani
Kwa mujibu wa Hadithi na maandiko ya Fiqhi  ya kisheria moja ya matendo maalumu ya siku hizi ni Dhikr ya Takbiir Allahu Akbar) baada ya Sala.

Masimulizi ya kihistoria yanataja matukio kadhaa makubwa yaliyotokea wakati wa siku hizo, Nazo ni pamoja na kisomo cha Surah Bira'at  sura ya Al-Tawbah kwa mahujaji wa Hija na Imam Ali (AS) kwa amri ya Mtume Mtukufu (SAW) katika mwaka wa 9 baada ya Hijra na kutiwa saini kwa Makubaliano ya Pili huko al-Aqabah, katika Siku ya pili ya Tashriq mwaka wa 13 baada ya Bi'thah na makubaliano haya na kundi la Ansari yalitayarisha njia kwa ajili ya Hijrah ya Mtume Mtukufu (SAW) kuhama kwenda Madina.

3488785

Kishikizo: mahujaji hija makka
captcha