IQNA

Taarifa ya Iran kuhusu uvamizi wa kijeshi wa Marekani dhidi ya vituo vya amani vya nyuklia vya Iran

19:40 - June 22, 2025
Habari ID: 3480851
IQNA-Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran imetoa taarifa ikilaani hujuma na uvamizi wa kijeshi wa Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya taifa hili vinavyofanya shughuli zake kwa malengo ya amani.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatambua haki yake ya kupinga kwa nguvu zake zote uvamizi wa kijeshi wa Marekani na jinai zinazofanywa na utawala huo, na kutetea usalama na maslahi ya taifa ya Iran.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalaani vikali hujuma za kikatili za kijeshi za Marekani dhidi ya vituo vya amani vya nyuklia vya Iran - ambazo zilifanywa kwa ukiukaji wa wazi na usio na kifani wa kanuni za kimsingi kabisa za Mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa - na inaitambua serikali ya Marekani inayochochea vita na inayovunja sheria kuwa ina jukumu na inabeba dhima ya athari na matokeo ya uhalifu huo mkubwa.

Uchokozi wa kijeshi wa Marekani dhidi ya umoja wa ardhi na mamlaka ya kitaifa ya Iran ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa - unaofanywa kwa uhalifu na ushirikiano wa utawala wa Kizayuni mtenda jinai kwa mara nyingine tena umedhihirisha kina cha uhalifu na uovu unaotawala sera za Marekani na kina cha uadui na chuki ya wasomi wa Marekani dhidi ya watu wanaopenda amani na wapenda amani wa Iran.

 

4290011

Habari zinazohusiana
Kishikizo: iran vita israel
captcha