IQNA

'Iran Mashallah!': Watu Saudi Arabia waisifu namna Iran inavyokabiliana na uchokozi wa Israel

19:06 - June 21, 2025
Habari ID: 3480850
IQNA-Waziri wa zamani wa Utamaduni wa Iran ameeleza jinsi Mahujaji wa kigeni na watu wa Saudia wanavopongeza jibu halali la Iran kufuatia uhokozi na uvamizi wa utawala haramu wa Israel.

Katika risala iliyoandikwa kwa Kiajemi kwa ajili ya Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), waziri wa zamani wa utamaduni wa Iran Ahmad Masjed-Jamei anasema:

Muamala wa watu wa Saudi Arabia, kama ule wa watu wa nchi nyingine, kwa Mahujaji wa Iran wakati wa Hija mwaka huu ni wa ukarimu na huruma. Ninakaa katika hoteli ambayo, mbali na sisi, kuna misafara mingine 19. Upande mmoja wa hoteli hufunguka kwenye barabara kuu, na mlango wa nyuma wa hoteli ni mahali ambapo bidhaa huletwa au kutolewa nje; mkabala na mlango huu, kuna msikiti wa mtaa huo ambapo wakati fulani mimi huenda kwa sala ya Adhuhuri. Kitongoji hiki kina wakazi wengi ambao ni wahamiaji-wafanyakazi kutoka nchi mbalimbali ambao wamefika hapa na kufanya kazi tofauti.

Baada ya kuanza kwa vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, kila ninapotembelea msikiti huu mdogo, ninashuhudia hali ya huzuni na mshikamano kati ya waumini walio hapo na Wairani. Kwa mfano, kabla ya swala, watu wanafuatilia kwenye simu zao za mkononi habari za namna Iran inavojihami kijeshi dhidi ya utawala wa Israel. Wanaruka ripoti na habari zingine lakini wanazingatia kwa uangalifu habari za punde kabisa namna Iran inavojilinda. Baada ya sala, nyakati fulani wao huandaa mlo  sahali unaojumuisha tende, maji, na mkate. Wanaotazama habari hizo huwa na furaha wakati wanapoona Iran imefanikiwa kuuadhibu kijeshi utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kuna Haji kutoka Kashmiri ambaye anaichukulia Kashmir kuwa Iran ndogo na anazungumza Kiajemi. anaelezea mapambano ya Iran kama "chanzo cha fahari kwa ulimwengu wa Kiislamu."

Watumishi kenye Masjid al-Haram pia wanaunga mkono Iran. Kufuatia upanuzi wa Haram wakati wa enzi ya Bin Salman, njia mpya za kuingia msikitini zimeundwa. Kwa kawaida, Wairani huingia kupitia Bab al-Ali. Siku moja, tulipoingia kutoka njia tofauti, nilimuuliza mmoja wa watumishi wa msikiti ni upande gani wa lango lile. Akauliza, "wewe ni Muirani?" kisha akaendelea: “Iran, Mashallah!” alijibu kwa furaha, “Milango yote ni Bab al-Ali.” Kauli yake ilinifurahisha, na nikamshukuru.

Siku moja, nilikuwa kwenye basi nikielekea Haram kwa ajili ya ibada. Dereva alikuwa Mmisri; Nilianza mazungumzo naye, na kwa uchangamfu na upole, alizungumza kuhusu Iran yenye “nguvu” na “Mujahid”. Alikuwa ameshika Tasbihi mkononi mwake. Nilimwambia kwamba Tasbihi yake nikama zile za Mashhad. Alijua Mashhad ya Iran. Akasema, “Kwa Tasbihi hii ninafanya Dhikr  kila siku, na nimekuwa nikitama kwa ajili ya Wairani kwa siku chache sasa.” Nikauliza, "Dhikr gani?" Akajibu, “Mara 33 ‘Allahu Akbar,’ mara 33 ‘Subhan Allah,’ na mara 33 ‘Subhan Allah wa bihamdih’. Nikamwambia sisi pia tuna dhikr hii, inayojulikana kama Tasbih ya Bibi Fatima (SA), lakini badala ya ‘Subhan Allah wa bihamdih,’ tunasema ‘Alhamdulillah.’ Akasema, “Ni vizuri sana kwamba mumeiba dhikri dhikri hii jina la Bibi Fatima (SA). Wamisri wanampenda sana Bibi Fatima (SA), binti ya Mtukufu Mtume (SAW). Misri, kila Mungu anapombariki mtu kupata watoto mapacha, huwaita Hassan na Hussein."

Mifano kama hiyo inaweza kuwa mingi.

Utawala wa Israel ulianzisha uchokozi dhidi ya Iran tarehe 13 Juni kwa kuyalenga maeneo ya makazi na kijeshi na kuwauwa makamanda wakuu wa kijeshi na wanasayansi wa nyuklia ambao hawakuwa kazini pamoja na familia zao. Mashambulizi hayo pia yalilenga vituo vya amani vya nyuklia vya nchi hiyo.

Iran, kwa kujibu, imezindua Operesheni ya Ahadi ya Kweli III, inayolenga miundombinu ya kijeshi ya utawala dhalimu wa Israel kwa makombora na droni au ndege zisizo na rubani

4289594

Habari zinazohusiana
Kishikizo: iran vita israel
captcha