Pir Hossein Koulivand, Mkuu wa Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, zaidi ya matabibu na wataalamu 7,000 wa fani tofauti za matibabu wamejitolea kutumwa Lebanon.
Wako tayari kwenda katika nchi hiyo ya Kiarabu na kujiunga na juhudi za kuwasaidia watu waliokumbwa na vita huko, alisema.
Koulivand pia amebainisha kuwa katika kipindi cha siku kumi zilizopita, wananchi wa Iran wamechangisha rial bilioni 40 kupitia Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran ili kuwasaidia watu wa Ukanda wa Gaza, Yemen na Lebanon.
Wimbi la mashambulizi ya anga ya Israel katika maeneo makubwa ya Lebanon yameua maelefu ya watu wakiwemo wanawake na watoto katika kipindi cha wiki chache zilizopita.
Watu wengi pia wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na hujuma za utawala ghasibu wa Israel.
4240921